Asilimia kubwa ya wanawake kwa wanaume kwa sasa wanasukia rasta, ni namna moja ya ku-protect nywele zako asilia lakini pia kuonekana mtanashati. Lakini mara nyingi baada ya kusikia rasta tunapatwa miwasho, hii ni kutokana na kemikali zilizopo katika rasta hizo tulizosukia. Lakini unaweza kuepukana na hali hii endapo tu utaziandaa kwa kuziosha rasta zako kabla ya kuzisukia.
Uwe na nini ili kusafisha rasta zako?
- Apple Cider Vinegar
- Maji Ya Moto
- Bakuli / Beseni Kubwa
Namna Ya Kuzisafisha
- Unatakiwa kuchanganya apple cider vinega na maji yako ya moto katika bakuli au beseni lako, kama ukiweka kifuniko kimoja cha apple cider basi utatakiwa kuweka vikombe vitatu vya maji ya moto hakikisha unaweka maji ya kutosha ili rasta zako kuweza kulowekeka vyema.
- Ziloweke kwa dakika kumi na tano (15), usitoe rubber band wala usijaribu kuzichana ziingize kwenye maji kama zilivyo ili usiziharibu ukashindwa kuzisukia, baada ya dakika kadhaa utaona vitu vyeupe juu ya maji vikielea, hio ndio kemikali inatoka.
- Baada ya dakika kumi na tano toa rasta zako na zikaushe kwa hewa ( airdry) usijali kuhusu harufu itaisha pale rasta zitakapo kauka vyema, lakini pia hakikisha zimekauka vyema kabla ya kuzisukia.
- Baada ya hapo unaweza kuzisukia kama kawaida.
Related posts
3 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Information on that Topic: afroswagga.com/hair/namna-ya-kuandaa-rasta-zako-kabla-ya-kuzisukia/ […]
… [Trackback]
[…] Find More here on that Topic: afroswagga.com/hair/namna-ya-kuandaa-rasta-zako-kabla-ya-kuzisukia/ […]
… [Trackback]
[…] Find More on that Topic: afroswagga.com/hair/namna-ya-kuandaa-rasta-zako-kabla-ya-kuzisukia/ […]