Katika Kila nguo huwa na lebo kwa ndani chini kidogo ya kola au pembezoni lebo ambayo huashiria maelezo ya kuitunza nguo hiyo ila wengi wetu huwa hatujui maana ya alama hizo, sio nguo zote huwa na maelezo ya alama nguo zingine huwa na maelezo tu japokuwa huandikwa kwa lugha kingereza au nguo zingine utakuta lugha tofauti inategemea imetengenezwa nchi gani. Japokuwa nyingi hutumia lugha ya kingereza.
Utunzaji wa nguo unaanzia kwenye Kufua, Kuipiga pasi na kuianika, lebo hizo zitakueleza unahitaji aina gani ya maji kufua nguo hiyo kama ni maji ya baridi au uvuguvugu. Unahitaji mashine au kufua kwa mkono, Upigaji wa pasi kama ni moto mkubwa, wastani au mdogo kabisa na kuianika kama ni juani, kuianika kwenye kamba au kuitandika sehemu tambarare. Kila nguo iko na masharti yake.
Je? Umeshawaza hawa madobi wa mitaani wanajua taratibu hizi za matunzo ya nguo au tunatumia mazoea kufua nguo zetu. Usilalamike nguo yako inapauka unajua taratibu za kuianika nguo hiyo? Mara nyingi nguo inayotoa Rangi inatakiwa kuanikwa sehemu ambayo haina jua ili kuzuia mpauko huo. Kwani sio jua pekee hukausha nguo hata upepo. Nguo za rangi nyeusi zinashauriwa kuanikwa sehemu ambayo haina jua sana au hakuna jua kabisa.
Aina ya maelezo hupatikana kwenye lebo za nguo .
- Dry Clean Only – Ufue kwa mashine za kufulia tu
- Do not Dry Clean – Usifue kwa Mashine za Kufulia
- Do Not Bleach – Usitumie Dawa za kutoa Madoa
- Do not Iron – Usipige pasi
- Low Iron – Piga pasi kwa Moto mdogo
- Do not Wring – Usikamue nguo hiyo
- Dry in Shade – Anika kwenye kivuli (hii kwa nguo ambazo hupauka zikianikwa juani)
- Tumble dry – Unaweza tumia mashine ya mvuke kukausha nguo hiyo
- Hand Wash – Fua kwa Mkono
- Mashine wash Normal – Unaweza kutumia mashine ya kufuli
Related posts
2 Comments
Leave a Reply Cancel reply
You must be logged in to post a comment.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Information to that Topic: afroswagga.com/lifestyle/maana-ya-alama-zilizopo-katika-lebo-za-nguo/ […]
… [Trackback]
[…] Find More Information here to that Topic: afroswagga.com/lifestyle/maana-ya-alama-zilizopo-katika-lebo-za-nguo/ […]