Weekend ime fika una muda mwingi wa kufanya mengi ambayo ulikuwa ukitaka kufanya lakini ukashindwa kutokana na ratiba ime bana katika siku za kazi au shule, tumia wakati huu kuziba yale mapengo ambayo uliyaacha katika siku zako za kawaida,

Nenda Mbali – inawezekana siku za kawaida una kimbia sehemu ndogo jaribu kukimbia mbali zaidi au kufanya mazoezi mara mbili ya unavyo fanyaga siku za kawaida kwa sababu una muda wa kufanya hivyo.

Ziba Mapengo – inawezekana siku za kazi huwa una fanya mazoezi machache ili ku manage muda, weekend una muda mwingi wa kukaa idol jaribu kutumia muda huo kuziba mapengo ya yale mazoezi mengine ambayo ulishindwa kuyafanya katikati ya week.

b8ff195f10391f6e_10729246_355459761287415_630501519_n.xxxlarge

Jaribu kufanya mazoezi mengine – panda milima, jaribu kufanya yoga fanya mazoezi ambayo huja wahi kufanya na jaribu kufanya mazoezi kwa kile kitu unacho hisi kinahitaji kipungue au kiongezeke mwilini mwako.

Jumuika na marafiki – siku za kawaida ni mara chache kupata kufanya mazoezi kwa pamoja, jaribuni ku jumuika kwa pamoja siku za weekend hii itasaidia kupeana motisha.

Comments

comments