Wengi tuna jiuliza hili swali Je naweza kuwa mwanamitindo hata kama mimi ni mfupi? Wengi wetu tunakatishwa au kakataa tamaa bila ya kusoma au kujaribu kiundani Zaidi. Jibu ni ‘NDIO’ Unaweza kuwa mwanamitindo hata kama wewe ni mfupi. Hukiachana na kuwa mwanamitindo wa kutangaza bidhaa kwenye barabara (runway) unaweza kuwa mwanamitindo wa vipodozi wakatumia uso wako tu, au kucha wakatimua vidole tu, au viatu waka tumia miguu tu lakini pia hata kwenye barabara inawezekana.
Inawezekana endapo tu kama mwanamke alie chini ya futi 5’5 akijua mipaka yake na Uwezo wake, akijua uwezo wake upo wapi ana weza kuwa mwanamitindo mwenye mafanikio makubwa Zaidi.
JINSI YA KUFANYA:
- JIPIGE/PIGA PICHA CHACHE ILI UONE MAJIBU YA LENS (LENZI YA KAMERA)
Uso na uwezo wako wa kucheza nao mbele ya kamera ni funguo/sifa mbili ambazo mawakala wa mitindo wanaangalia kwanza. Fikiria kupiga picha kitaaluma zaidi. Picha za kitaaluma zinaweza kuwa ghali zaidi lakini zita saidia zaidi kujua una tafuta nini au una kosea wapi. Pia utazihitaji hizi picha katika mahojiano ya kutafuta kazi kwaio zina thamani katika kuwekeza.
2) FANYA UTAFITI JUU YA MAWAKALA WA MITINDO
Pitia Tovuti zao na angalia wanamitindo wanao watumia ili kujua jinsi gani unaweza ukawa na nafasi ya kuchaguliwa. Kuwa makini katika wanamitindo wenye kimo sawa na wewe halafu linganisha vipimo vyao na vyako. Kuna mawakala ambao wana wawakilisha wasichana walio na kimo chini ya 5’5 lakini hawapendi kujulikana.
3)TAFAKARI MAAMUZI YAKO
- Fikiria kwenda nchi nyingine kutimiza ndoto zako bara kama Asia wana tumia mwanamitindo walio chini ya futi 5’6 inaweza ikawa rahisi kupata kazi huko
- Angalia upepo nje ya ulipo kuwepo na pia ni vizuri ukaanzia chini kabisa/kwenye msingi kwenda juu. Pia unaweza kupata uzoefu ukianzia chini.
ITAENDELEA……
Related posts
3 Comments
Leave a Reply Cancel reply
You must be logged in to post a comment.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Read More Info here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/1052/ […]
… [Trackback]
[…] Read More on to that Topic: afroswagga.com/mitindo/1052/ […]
… [Trackback]
[…] Read More to that Topic: afroswagga.com/mitindo/1052/ […]