Ni Siku Nne tu toka tuanze mwaka mpya, na tunaweza kusema mwaka tayari unaonekana kuanza vyema kabisa as watu maarufu mbalimbali wameonekana ku-slay na outfit zao.
Tunaanza na mwanamitindo Happiness Magese ambae alisheherekea siku yake ya kuzaliwa akiwa amevalia tulle dress ya pink akiwa amemalizia muonekano wake na pink open sandals, huku kichwani akiwa na low cut blonde hair.
Lakini pia tulikua na mwanamitindo mkubwa mwingine Milliam Odemba ambae yeye nae alikuwa in pink dress kutoka kwa mbunifu @fouadsarkisofficial yeye alimalizia muonekano wake na white & silver open sandals, dropped earrings na yeye alikuwa na blonde low cut.
Wengine ambao tuliwaona walipost picha zao wakiwa wameanza mwaka wao na slayage ni Fahyma ambae yeye alivaa colorful dress kutoka kwa @allie_clothings, amemalizia muonekano wake na gold heels.
Lakini pia mwanadada Sanch ambae kwa sasa anaenda kwa jina la Surraiya, yeye alivalishwa na mbunifu @elisha.red.label, ilikuwa ni pencil dress iliyoonyesha curvy zake vyema kabisa huku wakiwa wamemalizia na stylish cover up.
Tulikuwa na couple ya Ben Pol na Enerlisa ambao wao walikua in sequin fits, Enerlisa alivaa sequin black mermaid dress huku mumewe Ben Paul akiwa kwenye gold sequin coat suit aliyo match na gold bow tie akamalizia muonekano wake na black everything
Wakati wengine wote wakiwa wametoka occasional mwanamuziki Marioo yeye alituonyesha namna ya ku-slay in monochrome casual, akiwa amevalia kakhi two pieces ambazo alimatch na kofia yake amemalizia muonekano wake na white kicks.
Well Mates tuambie ni nani amependeza zaidi katika hii list?
Related posts
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…