Wenzetu wanaziita leggins sisi huku huwa tunaziita tight, ni moja ya vazi ambalo linapendwa lakini pia nirahisi kulivaa hasa kwa wale wapenda kuvaa casual.
Mara nyingi huwa tunavaa vazi hili katika mizunguko ya kawaida, na huwa hazichukulii kama vazi ambalo linaweza kuvalika vizuri na ukatoka nalo sehemu mbalimbali, leo tunakuletea namna nyingine ambazo unaweza kuvaa na ukaonekana stylish.
Namna moja wapo ya kunyanyua vazi hili ni kuvaa na vitu sahihi, how you style it ndivyo ambavyo vazi lako litapendeza zaidi
Kama una mizururo tu ya kawaida badala ya kuvalia leggins na sandals za kimasai au sandals za manyoya chagua classic sandals, pia accessories vyema na kama ni shirt au t-shirt unayovalia juu basi iendane na kimoja kati ya pochi au kiatu unachovaa lakini pia unaweza kuvaa shirt na leggins za rangi moja na ukapendeza.

na kama ni mtoko wa usiku basi upgrade muonekano wako accodingly, kama ni mpenzi wa heels valia na heels, accessoriez na pochi nzuri, miwani na hata kuongezea blazer au classic top kwa juu ili kunyanyua muonekano wako.

Tukutakie weekend njema.
Related posts
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…