Moja ya trend kubwa sasa hivi ni oversized shirts, unajuaje kama ni trend? Angalia namna ambavyo maduka ya mavazi yana-stock hizi shirts, na ambavyo watu wengi wanayavaa, tunaweza kusema ni trend yetu pendwa kwa maana inaweza kuvaliwa na yoyote lakini pia unaweza kuvaa mara nyingi uwezavyo kutokana na sehemu unayoenda na namna ambavyo unaweza ku-style trend hii.

Well leo tunakuletea namna mbalimbali ambavyo unaweza ku-style over sized shirt weekend hii:

Over sized Shirt With Biker Shorts

Moja kati ya namna unaweza kuvaa trend hii ni kuvalia na biker shorts, ni rahisi na ni fashionable hakikisha unapangilia rangi zako vyema na kuvalia viatu ambavyo upo comfortable navyo, kama unaenda for a more casual look basi raba, flat’s au boots zitafaa zaidi lakini kama ni mitoko muhimu unaweza kuvalia na heels. Kama haupo comforable na biker shorts unaweza kuvalia na tight ndefu.

Over Sized Shirt With Denim Shorts

Yes kama unapensi yako ya jeans unaweza kuvalia na over sized shirt pia, mchawi ni namna ambavyo una style vazi lako, unaweza kuchomekea upande mmoja, kuvalia kama cover up juu etc. na kama haupo comfortable na shorts unaweza kuvalia suruali ya jeans.

Over Sized Shirt With Skirt

Hii ni moja ya namna nyingine unaweza kuvaa oversized shirt yako na ni namna tofauti kabisa ambayo itakufanya uonekane unique & sexy kama unaenda brunch au dinner au date inafaa zaidi.