SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Jinsi Ya Kutambua Umevaa Fake Clothes
September 19, 2018: Milan, Italy - Street style outfits in detail during Milan Fashion Week - MFWSS19
Mitindo

Jinsi Ya Kutambua Umevaa Fake Clothes 


una baadhi ya vitu vinatokea kwa kujua na kutokujua unamkuta mtu kanunua nguo expensive lakini ni fake sio tatizo lake hilo kwa sababu alikuwa hajui. Leo tunakuletea tips zaidi ya kujua umevaa fake clothes au lah.

Zipo njia nyingi sana za kujua kwanza anza na hizi tips

1.  Jua majina ya brands za nguo 

Katika kitu muhimu cha kwanza unachotakiwa kufanya ni kujua majina ya brands za nguo kwa sababu kila brands ina jina lake kwa mfano unataka nguo aina ya gucci then unaenda dukani unakuta nguo imeandikwa gucck then unanunua hapo utakuwa umenunua nguo fake. Jitahidi sana kujua kila herufi ya hiyo brands husika ambayo unataka kwenda kununua kwa sababu watu wanaotengeneza nguo fake wanabadilishaga kitu kidogo sana unaweza ukakuta pattern na kila kitu kipo sawa kasoro jina tu.

2.  Zingatia aina ya kitambaa

Katika kitu ambacho hawawezi kuwa the same na real brands basi ni kwenye aina ya kitambaa mara nyingi sana fake clothes zinakuwa na kitambaa tofauti sana na nguo original kwa hiyo kila ukienda kununua jitaidi sana kujua aina ya fabric ni sawa na original.

3.  Zingatia logo 

Unaweza usiamin sana ila logo za brands huwa wanazitofautisha sana ndo yale mambo ya kumkuta jordan kashika mic. Ukiweza kuzingatia logo basi utaweza kusave pesa yako na utakuwa umenunua nguo ambayo ipo katika kila kiwango na utaipenda kuivaa mda wote kwa sababu unajua umevaa nguo original.

4.  Zingatia bei 

Mara nyingi walimwengu husema vitu vizuri haviji kwa bei rahisi so kitu cha msingi zingatia bei. Tunaposema zingatia bei ni kwamba hauwezi pata gucci au levis kwa 1500 tshs. Ukiweza kujua real price basi itakuondolea kununua kitu ambacho hautokuja kuvaa kulingana na quality ya hiyo nguo.

5.  Fanya utafiti 

Unaweza ukadhani ni kitu kidogo sana lakini ukifanya utafiti basi itakuwa umenunua kitu kwa kupenda mwenyewe hata kama ni fake. Ukiwa na uwezo wa kujua bei na aina ya fabric utakuwa umejiondoa kwenye kununua nguo fake na utaoneka mjanja sana.

Note: tunajua mnapenda kuvaa brands ila zingatieni kuvaa vitu original kwa sababu inakuondoa kwenye kufanywa memes mitandaoni. Unaweza kutuambia ni nguo gani fake ulishawai kununua.

Imeandikwa na Gotchathegreatest

Related posts

1 Comment

  1. clindamicina en crema

    […] clindamicina en crema[…]

    clindamicina en crema

Comments are closed.