Umesha wahi kufikiria hawa stylist ambao huwa wana style wenzao wamekuzidi nini? au ni nini wanafanya mpaka wao wawe stylist na walipwe kuwa valisha wengine? lakini pia unaweza kuwaza ni vipi wao kila wanacho vaa wanapendeza? Well kuwa stylist si lazima usomee, styling is an art ni kama sanaa ambayo sio wote tunaiweza ni kama uigizaji, uimbaji au hata uchekeshaji n.k.
Leo tunakupa vitu vitatu ambavyo mara nyingi stylist hufanya na kuoekana ameleta utofauti katika muonekano wake au alim-style.
- Additional / Nyongeza
Tumezoe sisi kama ni skirt basi tutavaa skirt na blouse na viatu tumetoka, au jeans, T-shirt na raba tunatoka, stylist wapo tofauti kabisa ni lazima watafikiria kitu gani cha tofauti anaweza kuongezea kama accessories kama kuongezea belt au blazer katika muonekano wake yaani kuongezea kitu ambacho kita leta utofauti.
- Kufikiria Nje Ya Box
Stylist huwa wanafikiri nje ya box, anaweza akavaa shirt nyuma mbele ili mradi awe tofauti, aka chukua vazi ambalo ni casual akalifanya kuonekana official, wao kazi yao kubwa ni kuleta utofauti katika mavazi. Kuangalia jinsi gani anaweza kuchanganya rangi ambazo wengi hawawezi kuvaa.
- Statement
Stylist lazima wachague kitu kimoja ambacho kitafanya muonekano wao u-pop kama ni kuongezea colorful cloth, kiatu, pochi, statement jewelry ili mradi kuwe na kimoja au viwili ambavyo viatakufanya umuangalie mara mbili na upate cha kuongea anaweza akavaa full black outfit akaongezea na yellow shoes au red ambavyo vitaiba attention ya macho yako.
Sio rahisi lakini pia sio ngumu kama ukiwa unafuatilia hivi vitu vitatu kila siku wakati unataka kuvaa mavazi yako.
Related posts
HOT TOPICS
We need to have some sort of bima ila for enjoyment. Yaani wanakata ka % ka mshahara kako unakua na card ukienda se… https://t.co/W9oDoaN2YY
FollowSubscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…