SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

3 Tips Za Kuonekana Elegant Nyumbani
Mitindo

3 Tips Za Kuonekana Elegant Nyumbani 

Kuna wale wenzangu na mimi tukitoka tunawaka, nywele kali, ka-makeup usoni, tunanukia mpaka tunavutia majini lakini ukifika nyumbani tu hali inabadilika, wig imetupwa kushoto una mabutu yako yana miezi mitatu, unatoa nguo unachukua ki-khanga chako kimepaukaa, unukie au uoge unaenda wapi kwani? upendeze unam-pendezea nani? ukisikia hodi unanuna huyu nae nani mi niko hovyo lol, kama unavyoendelea kusoma ndio unajiona kabisa ni wewe na ungependa kuacha hii tabia basi hizi tips 3 zitakusaidia,

  • Fresh Up A Liltle Bit

Huitaji makeup ukiwa nyumbani lakini haimaanishi usiwe vyema, kuoga sio mpaka utoke oga vizuri,paka perfume, perfume sio tu kwa unaokutana nao bali hata kwako pia ukinukia vyema unajisikia vyema, chana nywele au suka minyoosho yako mizuri, fanya skin care, huwezi kupaka lipstick basi hata ka lip balm ka hapa na pale hakadhuru,

  • Upgrade Mavazi Yako Ya Kushindia Nyumbani

Mavazi ya ya kushindia sio ndio yawe yale yaliopauka ambayo unaona huwezi kutoka nayo nje, mgeni anakuja una khanga imechanika au t-shirt ya msiba toka mwaka juzi imefubaa, nunua mavazi mazuri ya kushindia nyumbani mfano lounge wear, two piece sets, leggins & tank top, tank dress, casual 2 pieces set etc

  • Upgrade Mavazi Yako Ya Kulalia

Hapa ni sawa tu na mavazi ya kushindia sio kwasababu unalala usiku basi ndio uvae mavazi hayaeleweki hata ukitokea moto usiku ushindwe kutoka nje, hakikisha mavazi yako ya kulalia mazuri na ni comfortable mfano satin payjamas, silk satin sleep wear inaweza kuwa gowns au set inategemea na mapenzi yako

Huitaji kununua haya mavazi kwa gharama kubwa unaweza kununua hata mtumba lakini yawe na quality nzuri.

Related posts