Ikiwa kwasasa wedding guest wanakwambia ukialikwa alikika na ukialika jiandae kwa maana kwamba kama mgeni umealikwa hakikisha una alikika kwa kupendeza vyema kabisa na kama wewe ndio umealika waje kwenye harusi yako hakikisha umejiandaa vilivyo ukilegea tu waalikwa wanapendeza zaidi kuliko mwenye sherehe, leo tumeona tuwaletee ukumbusho wa nini kinafaa kuvaliwa na nini hakifai kuvaliwa kama wedding guest,
- Usivae rangi nyeupe,cream au off white
Kama ambavyo tunajua hizi ni rangi ambazo maharusi wengi wanazitumia siku za harusi yao, inafaa kumuacha mwenye harusi a-shine huku sisi wengine tukivaa rangi nyingine ili kuweka utofauti na kuto kum-outshine muhusika, lakini kama ni theme ya harusi then ni ruhusa kuvaa.
- Usivae mavazi yanayo onyesha maungo sana
Hakikisha vazi lako ni la kistaarabu usiachie maungo kupitiliza, uzivae vazi fupi sana, usivae vazi linaloonyesha sana kifua kupitiliza, Usivae vazi linalobana maungo kupitiliza hii itafanya watu wakuangalie wewe na kupoteza attention kwa muhusika lakini pia ni mkusanyiko wa watu mbalimbali kila mmoja wetu ana imani zake usiwe kero kwa wengine.

- Usivae rangi / prints zinazo shout
Hii pia inasababisha attention iwe kwako na inawezekana ukawa out of theme na wengine hakikisha unavaa rangi nzuri calm zenye kuvutia unaweza kuvaa prints au rangi inayo shout endapo tu ndio theme ya sherehe.
- Usivae too casual
Kwa wale tunapenda kuwa kawaida tu unaweza kwenda kwenye harusi hata na jeans tuache kwa maana ile ni siku muhimu kwa maharusi unaweza kuvaa hivi kama maharusi wamesema uvae lakini kama hujaambiwa ichukulie uzito kidogo na uvae mavazi yenye kuendana na sherehe.
Related posts
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…