Tunaweza kusema miaka mitano ijayo kama Nigeria itaendelea hivi basi watakuwa mbali sana katika ulimwengu wa Fashion, Mara nyingi huwa tunasema mmoja anapo fanya kitu kikubwa huko Duniani si yeye anaesifiwa bali Nchi nzima na ndio maana utasikia A Designer From Nigeria au fulani kutoka Nchi fulani ndivyo ambavyo wenzetu wanafanya.
Ndani ya mwaka huu miezi saba tu toka mwaka uanze tumeshaona vitu vinne vikubwa ambavyo vimepeperusha bendera yao huko Duniani,
- Tiwa Savage Instagram Kutajwa Na Vogue Katika Account 10 Bora Zenye Fashion Creativity
- Account Ya Instagram Ya Tiwa Savage Yaingia Katika 10 Bora Kama Vogue Fashion Creativity Accounts
Mwaka huu February mwanamuziki kutoka Nchini Nigeria alitajwa na gazeti kubwa linalo aminika na watu mbalimbali Duniani la Vogue kuwa account yake ni moja kati ya accounts 10 bora za instagram zenye fashion creativity, linaweza kuonekana ni jambo dogo lakini ni kubwa mno, unapo soma kwamba Tiwa ametajwa utataka kujua kwanini katajwa? ana nini cha special kwenye account yake? anatokea wapi? Anapo tokea je kuna wabunifu au models wana fanya nini? vitu vingi ungependa penda kujua kuhusu yeye na hapa ndipo ambapo utaijua Nigeria kama Nchi na ubunifu wao, This is a step and it is a big step huwezi kushangaa kumuona Tiwa akiwa na Naomi Campbell kwa sababu she owned it through her fashion & music.
- Nigerian World Cup Jersey Took The World By A Storm
Kama hukuisikia ikiongelewa kwenye mitandao, Tv au sehemu yoyote do you real exist in this world? Nigeria wanaweza kuwa wametolewa kwenye mashindano ya kombe la Dunia but they real left a mark huko Duniani kupitia jersey yao, According to GQ magazine the jersey’s picked up an alleged three million pre-orders (more on that later), sold out at Supreme box logo speeds, and is now reselling like one of those BOGO tees on the secondary market. Three Million people wamevaa hii jersey ikiwa original tena ni pre – order sasa fikiri ambao walizinunua madukani na wale wenzetu na sisi wa kufyatua, Nigeria real made a big step hapa na tusisahau jinsi ambavyo walivaa mavazi ya ki-Nigeria siku wakiwa wanaondoka kwenda Russia. Hii Jersey ilitengenezwa na Kampuni ya Nike, Yes NIKE.
- Rapper Wiz Kid Ayo Kutembea Katika Runway Ya Dolce & Gabanna
- Wiz Kid Ayo Katika Runway Ya Dolce Gabanna Akiwa Na Naomi Campbell
Dolce and Gabbana ni kampuni kubwa ya mavazi na sio kila mtu tu anaweza kutembea katika runway yao, Rapper Wiz Kid’Ayo kutoka Nigeria mwaka huu alitembea katika Run Way yao huku akiwa ameambatana na mwanamitindo mkubwa Naomi Campbell, Wiz Kid alitembea katika runway hii akiwa amevalia collection ya Spring Summer 2019 ambapo ilikuwa debuted Milan, Nchini Italy. Nigeria did it again Wiz Kid made history kuwa msanii wa kwanza kutoka Africa kutembea katika Runway ya Dolce & Gabanna.
- Mbunifu Kutoka Nigeria Taofeek Abijako Kuonyesha Mavazi Yake Katika New York Fashion Week na Ndio Mbunifu Mdogo Zaidi Katika Historia Kufanya Hivyo
Guess anatokea Nchi gani? Nigeria. Nigeria wamekuwa waki make history tu mwaka huu kwenye ulimwengu wa fashion they don’t play, sio tu kwamba wana fanya hapana ila wana weka historia katika ulimwengu wa mitindo, Taofeek Abijako ana miaka 19 na ni mbunifu wa mavazi ya kiume, aya show case mavazi yake katika New York Fashion Week Mens Wear fall/winter 18.
Sisi bado tupo tukilalamika Tasnia ya Mitindo ni Ngumu.
Related posts
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…