Ni week nyingine tena inayoenda kuanza, umesha jiandaa na nywele, kucha, mentally uko tayari kabisa kuianza week yako lakini tunajua namna ambavyo inaweza kuwa hectic katika kuchagua nini uvae kwenda kazini.
Kama wewe ni mdada na unapenda kupendeza ila iwe kidada zaidi basi look hizi nne kutoka kwa Hamisa Mobetto zinaweza kukufaa
Matching set
Matching set ni vazi rahisi zaidi kuvaa ofisini, unaweza kuvaa kama set ilivyo au ukaamua ku-style piece mojamoja kama una muda lakini kama una haraka zako basi hii ni choice nzuri kwa Hamisa tumemuona na hii set ya top na pleated skirt ambayo alimalizia muonekano wake kwa kuvalia miwani, handbag na open heels

Statement Color Dress
Sio kwamba unaenda kazini basi mavazi yako yawe boring, unaweza kuvaa kigauni nyenye rangi yenye kuvutia na heels zako ukapendeza na kuonekana presentable ofisini, kama hapa tunavyomuona Hamisa akiwa amevalia hii blue dress ambayo alimalizia muonekano wake kwa kuvalia na white stiletto pamoja na kubeba handbag

Blazer Dress
Blazer dress ni classy na ni professional kama unapendakuvaa magauni basi hii hutakiwi kuikosa kabatini kwako, ni moja ya vazi ambalo ni rahisi kuvaa na ku-style na ambalo linakupa classy look. Urefu unategemea na comfortability yako kwa Hamisa tumeona amevaa ballerina Legth ambayo imesaidia kuonyesha skin na viatu.

The Jumpsuit
Namna nyingine rahisi ya kuwahi ofisini ni kuvaa jumpsuit, mix and match ya suruali au mabwanga huwa inachukua muda ila endapo utakuwa na jumpsuit au gauni zinazoeleweka basi itakusaidia kupunguza muda wa kuchagua u-match nguo ipi na ipi.

Ni matumaini yetu umepata idea ya nini uvae week hii ofisini, tunawatakiwa week njema.
Related posts
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…