SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

5 Wardrobe Essentials You Should Own
Mitindo

5 Wardrobe Essentials You Should Own 

Wengi tunashindwa kujua tuanzie wapi na tuishie wapi katika kununua mavazi,na hii inapelekea kuwa na nguo nyingi ambazo haziwezi kujirudia unavaa mara moja hujui uvae wapi tena, well leo tunakuletea vitu 5 muhimu kuwa navyo katika kabati lako ambavyo ni kama msingi wa kuelekea kuwa stylish & classic wear.

 • Plain White Tee / Shirt

T shirt au shati nyeupe ni muhimu kuwa navyo katika kabati lako, ni kutokana na kwamba inaweza kuvaliwa na chochote iwe suruali ya kitambaa, jeans, skirt, culottes, pensi nk, lakini pia inaweza kuwa casual na smart wear. Kabati lako si kamilifu kama bila ya kuwa shirt au t-shirt nyeupe.

 

 • Perfect Jeans

Iwe skin jeans, mom jeans, iwe flared au cropped ili mradi ni jeans ambayo ina ku-fit vizuri basi ni muhimu kuwa nayo, kizuri kuhusu jeans nazo ni moja essentials ambazo zinaweza kutumiwa zaidi ya mara moja kama ni mzuri wa ku-style unaweza kuvaa hata week nzima,casual na hata business wear. Kingine unaweza kuvalia flats au heels inategemea na chaguo lako.

 

 • Blazer

Hata kama hufanyi  kazi katika ofisi , kila mwanamke anapaswa kuwa na angalau blazer moja ambayo ina mtosha vizuri, kama haikutoshi sawia hapo ndipo itabidi utafute fundi wa kukurekebishia, blazer inakufanya uonekane well polished na mostly smart. 

Kwa upande wa viatu una paswa kuwa na

 • Viatu vurefu (Heels )

kila mwanamke anapaswa kuwa na angalau pear  mbili za viatu virefu Viwe ni pumps au strappy sandals. Viatu virefu vinakufanya uonekane jasiri, lakini pia vianakuongezea kimo. unaweza kuwa na pear hizo mbili za rangi nyeusi na nude. lakini kwa wanawake huwa hatuna enough shoes unaweza kuwa nazo nyingi uwezavyo.

 • Ballet Flats 

Kuna sababu kila mtu anapenda kuvaa ballet flats, vinakufanya uonekane chic & smart . Unaweza kumiliki viatu hivi kwa rangi mbalimbali pia unaweza kuvaa  na jeans na mavazi tofauti tofauti, kikubwa ni kwamba ballet zipo comfortable & rahisi kutembelea.

 

Related posts

2 Comments

 1. MAA Streams

  … [Trackback]

  […] Read More Information here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/5-wardrobe-essentials-you-should-own/ […]

 2. buy weed online mississauga

  … [Trackback]

  […] Find More on on that Topic: afroswagga.com/mitindo/5-wardrobe-essentials-you-should-own/ […]

Comments are closed.