Alisha wahi kuwa Miss Ubungo, Akaja Kuwa Miss Kinondoni na mwaka 2004 akaja kukwaa taji la Miss Tanzania Anaitwa Faraja Kotta mwanadada/Mwanamama ambae warembo wengi wanao shiriki mashinda ya urembo na hata ambao hawapo kwenye urembo wanamuangalia, hii ni kutokana na yeye ku-manage kukaa kwenye peak yake hata baada ya Miss Tanzania, Faraja hajihusishi na maswala ya urembo kwa sasa ameolewa lakini pia ni Kotta ni Mwachama wa “Youth Executive Committee” ambayo ipo chini ya Youth Net Tanzania, na pia ni Program Officer wa kipindi cha Njia Panda ambapo anafuatilia wale wananchi wanaojitokeza na matatizo na kuhakikisha wamesaidiwa na vipi wanaendelea.
Kutokana na yeye kutokuwa kwenye urembo tena lakini bado ana heshimika na bado anafanya kazi za kusaidia wengine, lakini pia kuweza kujiweka professional na maisha yake hata baada ya kuvua taji la Miss Tanzania imetufanya tumtafute tuweze kupata tips za vipi hawa beauty pageant wa sasa wanaweza kuwa kama yeye na hii ni kutokana na kwamba wengi wao huwa wanaishia hewani baada ya Miss Tanzania
Afroswagga – Kutona na kuibuka wimbi kubwa la Beauty Pageant Winners Kuishia Hewani Baada Ya Kuvua Taji Hilo Je Unaweza Kutupa Tips chache kwa hawa upcoming beauty Pageant kufika mbali bila kutumia mitandao au miili yao vibaya?
Faraja – Kikubwa kwa mtu yeyote ni kuwa na malengo yatakayoamua nini afanye kufikia malengo yake. Kama beauty queen usipokuwa na malengo yako binafsi basi jamii itakupa malengo waliyo nayo juu yako. Itakuongoza uweje, uvaaje na ufanyaje kazi na hapo ndipo umaarufu unaanza kupumbaza, Kwahiyo tips chache:
1. Tambua thamani yako na amua unataka nini kwenye maisha yako
2. Usisahau wewe ni nani – na mara nyingi wewe ni muunganiko wa watu wengi, usiwasahau, usijiangushe na usiwaangushe
3. A new star is born every day, fame is an illusion
4. Hakuna kitu kibaya kama kuiga mtu mwingine kwasababu inamaanisha hujipendi
5. Tabia zinatengenezwa hatuzaliwi nazo, tafuta tabia njema, badilika ikibidi
6. Kuna fursa nyingi iwapo utaamua kuzingatia, kwakuwa beauty queen tayari una jukwaa la kuanzia, inakupa utambulisho kirahisi tofauti na vijana wengine ambao hawapo kwenye burudani, use this opportunity well. Hata hii fursa ni ya muda, pia itafunga. Ikifika wakati inafunga inabidi iwe imeshakunyanyua kwenda level nyingine
Tulicho muelewa ni kwamba wakati upo kwenye peek au bado hujavua taji lako jaribu kutafuta fursa kwamba hata ukishalivua unajua kuna hiki naweza nikakiendeleza baada ya hapa. kila kitu kina mwisho usilewe kuwa wewe ni Miss Tanzania basi utakua hivyo milele ni kweli utakua katika kumbukumbu ya List za walio wahi kuwa Miss Tanzania au beauty pageant nyingine lakini Je ulifanya nini baada ya hapo? Jijengee misingi ya baadae.
Related posts
1 Comment
Leave a Reply Cancel reply
You must be logged in to post a comment.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Read More Info here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/6-tips-from-former-miss-tanzania-faraja-nyarandu-to-upcoming-beauty-pageant/ […]