Anaitwa Johary Jafary wengi tunamjua kwa jina la JouJou Nyaki ni stylist ambae amesha wa style watu maarufu kadhaa akiwepo Vanessa Mdee
Mimi Mars na wengineo wengi, Joujou yupo tofauti na stylist wengine wengi ana style unique sana she is bold & colorful hakimbii rangi tofauti na wengine hili ni moja kati ya mengi yaliyo tuvutia kwake, tumepata nafasi ya kufanya mahojiano na stylist huyu tumepata kujua na kujifunza mengi kutoka kwake
Afroswagga – Tuambie kuhusu wewe na kazi yako, ni vipi ulianza/kuamua kuwa stylist?
Joujou Nyaki – Kwa jina naitwa Johary Jafary a.k.a Joujou, owner of Joujou House of Style.
Biashara yangu ina deal na kuuza nguo, viatu, pochi na accessories nyingine lakini ninajulikana zaidi kama Stylist. Styling nilianza tangu niliyoanza kuwa msichana nikiwa ya secondary. Toka wakati huo nilikuwa na utundu na mavazi na nilipenda kuonekana tofauti hata kwenye uniform za shule. Kwa mfano, kama uniform inatakiwa kuwa ya rangi ya kijani basi mimi nitaongeza utundutu wangu na kuchagua kijani iliyoiva kidogo lakini bado inakuwa imekubalika kama rangi ya shule ilimladi tu niwe smart na kupata muonekano mzuri wa tofauti. Kwa sababu hii hata wanafunzi wenzangu walitaka kutengeneza nguo sawa na mimi. Wakati wa zile disco za shuleni nilikuwa nahakikisha navaa vitu unique na stylish, yaani kila disco wenzangu walikuwa wana subiri kuona nitavaa nini. Hiyo ikapelekea wanafunzi wenzangu kuona kwamba Joujou ana kipaji kwenye kupangilia mavazi na wao wakaanza kuniomba niwapangilie mavazi yao kwa kila disco za shule. Niliamua kufungua Joujou House of Style mwaka jana na nikaanza kuvalisha wasanii kama NavyKenzo. Mpaka sasa hivi nimeshavalisha wasanii wengi, lakini vilevile nafanya kazi na watu wa kila aina katika Styling pamoja na kuuza nguo n.k
Afroswagga – Tuelezee (describe) style yako kwa maneno matatu
Joujou Nyaki – *colorful
* unique (stands out)
*trendy
Afroswagga – Tunapo pitia page yako style yako vibrant, colorful cloth, vijikofia fulani etc je ndio signature style yako?
Joujou Nyaki – Naweza kusema unachokiona kwenye page yangu ni part of my signature kwa sababu kama nilivyo describe my style hapo juu ni trendy kwa hiyo inabadilika na wakati, haiko fixed. Ninachopenda kufanya ni kuonyesha different ways to wear certain items kama hizo kofia, colors n.k. Also nowadays fashion is cyclical and changes very fast, maana hata vitu vya zamani huwa vinarudishwa with a different and modern touch na mimi ni mfuatiliaji sana wa fashion worldwide, kwa hiyo huwa napenda kuwaonyehsa watu new trends ambazo mtu ambaye hafuatilii sana fashion anaweza asijue. Kwa hiyo, nawashauri watu wani follow @joujou_nyaki03 na @joujouhouseof style iliwapate tips za kuvaa, wanunue item ambazo zipo on sale pamoja na kuni book for styling.
Afroswagga – Kama stylist huwa unatumia mavazi kutoka kwa wabunifu wa Tanzania? Ndio Nani? Hapana Kwanini?
Joujou Nyaki – Mimi napenda kufanya kazi na wabunifu wa ndani kwa sababu inanipa fursa ya ku-create something from scratch na hivyo naweza kuonyesha ubunifu wangu zaidi, pamoja na kwamba suala la Stylist na Wabunifu kushirikiana bado ni jipya kidogo. Kwa kiasi kikubwa sasa hivi kila mmoja anafanya kazi kivyake. Ni matumaini yangu hali hii itabadilika na kutakuwa na ushirikiano wa kikazi kati ya Stylist na Wanamitindo kwa sababu naamini itakuwa na manufaa kwa wote. Mimi kwa upande wangu nimeanza kushirikiana na Mbunifu chipukizi mwenye talent sana anaitwa Saleh ambaye pia anamvalisha Lilian Masuka wa kipindi cha Storm on Clouds TV.
Afroswagga – mbinu yako ya kwanza unapotaka kumstyle mtu Je unamuuliza maswali anapenda kuvaa nini au huwa unapitia kabatini kwake?
Joujou Nyaki -Mimi mara nyingi napenda kwanza kusikiliza matakwa ya mteja wangu alafu nakwenda kuangalia closet yake. Lakini another part of the process ni kujua hilo vazi ni kwa ajili ya tukio la namna gani, is it a wedding, award show, music video, dinner event, beach party etc., vilevile ni muhimu kuzingatia umbri na body style ya mtu.
Afroswagga – The Must Haves Accessory kila msichana ana paswa kuwa nazo?
Jaoujou Nyaki – *Sunglasses
*Earrings
*Neckless
*Lipstick
*Purse
*Smart Phone
Afroswagga – Msanii gani ulipenda sana kufanya nae kazi kati ya wote ulio wa style na nani ungependa kumstyle siku zijazo?
Joujou Nyaki – Here I will break the rules and have to name two (sisters)
nimependa kufanya kazi na Venessa Mdee na Mimi Mars. Msanii ningependa kufanya naye kazi ni Wema Sepetu.
Afroswagga – Vitu pendwa kabisa katika kabati lako ambavy havikosekani? (Favorite items in your closet)
Joujou Nyaki -*Denim jeans, Jump Suit, Blazer jacket, Baseball cap, T-shirts, Black tights
Afroswagga – Trend ambayo hutokuja kujaribu kuivaa?
Joujou Nyaki – You can never say never in the fashion world, fashion is limitless, so since they say fashion has no limit i wil try every thing and make it the best look in fashion eye
Afroswagga – unadhani kwanini watu maarufu wa Tanzania hawashirikishi ma stylist katika kuchagua mitoko yao na nini kifanyike?
Joujou Nyaki – Mimi nadhani watu maarufu hawashirikishi stylist 1) kuogopa gharama wanadhani uenda kuna gharama kubwa kuwa Na stylist 2) wanaona kwamba labda wao wanajua kuji style 3) ni kitu kipya kwa nchini kwetu kutambulika kama profession yenye kuongeza thamani kwa Msanii au mtu yoyote na kuweza kubadilisha muonekano wako.
Afroswagga – Chochote Ambacho ungependa kuwaambia wa Tanzania
Joujou Nyaki – Mimi ningependa kuwaambia watanzania wenzangu muonekano wa mtu una nafasi kubwa sana kwenye kujitambulisha vizuri kwa jamii, as they say ” you don’t get a second chance to make a first impression”. Nawashauri watanzania wenzangu waone umuhimu wa kutumia Stylist kama ni waigizaji, wanamuziki, watu wa maofisini na pia watu wa kawaida
Kama ungependa kuwasiliana na Joujou Mfollow Instagram @joujouthestylist .
Related posts
3 Comments
Leave a Reply Cancel reply
You must be logged in to post a comment.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Find More Info here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/a-talk-with-joujou-nyaki-the-stylist/ […]
… [Trackback]
[…] Read More on that Topic: afroswagga.com/mitindo/a-talk-with-joujou-nyaki-the-stylist/ […]
… [Trackback]
[…] Read More Information here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/a-talk-with-joujou-nyaki-the-stylist/ […]