SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

A Touch Of Color Of The Year – Lavender
Mitindo

A Touch Of Color Of The Year – Lavender 

Ultra Violet 18-3838 ndio ilitangazwa kuwa rangi ya mwaka 2018, japo haikukiki sana mwanzoni lakini kwa sasa kila fashionista ana jaribu kuonyesha umahiri wake katika kustyle na kuvaa hii rangi. Kuna wale ambao wanavaa head to toe lavender na kuna wale ambao wanaonyesha ujuzi wako kwa kuchanganya rangi hii na rangi nyingine, we are here for it.

Wachaguaji wa rangi hizi Pantone wameeleza kuwa  kuwa ni rangi yenye kumaanisha upekee kwa kila mtu yenye kusimamia uhalisi, uelekevu na usawa kwa watu. Rangi yenye mfanano na anga za mbali katika sayari (galaxies) hivyo kumaanisha chochote chawezekana na yenye kutupeleka in the future.

Unaweza kuangalia hapo chini namna fashionista’s walivyokupa ideas za namna ya kustyle rangi hii

  • Lavender suit na stripes

tumemuona fashion blogger mimigstyle akiwa  amevalia suit ya rangi hii ambapo yeye alichanganya na top ya mistari nyeusi na nyeupe akamaliza na viatu vyenye rangi hii ya kukoza na miwani na drop earrings, tunaweza kusema hii rangi imetulia mno unaweza vaa vyovyote ikakubali.

  • purple feathers

mwamamuziki Cardi B yeye alionekana katika Paris Fashion Week akiwa amevalia hii extra jumpsuit ya purple ikiwa na feathers amemaliza muonekano wake na nywele zenye rangi sawa na suit na viatu vya silver. Yes Cardi slay on them

  • Pant It

Kama hupendi kuwa full Lavender unaweza kuchagua kuvaa moja kati ya suruali, skirt au top ya rangi hii ku represent for the culture

  • color blocking

Jacqueline Mengi ametuonyesha how its done kuvaa rangi hii kama top huku ukiwa umechanganya na rangi nyingine, she shine’s bright.

 

wakati blogger style pantry yeye akitupa date night outfit idea akiwa amevaa rangi hii na rangi ya njano, we feeling it.

Well hii ndio rangi inayo kiki kwa sasa ukiachana na neon colors, unaweza kujaribu kuvaa na usisite kututag kama utafanya hivyo

Related posts