Afroswagga Fashion Awards kama zilivyotambulishwa ni jukwaa jipya ambalo limekuja kwa lengo moja mahsusi ikiwa ni kuthamini mchango wa wadau mbalimbali katika tasnia ya mitindo na urembo. Inafahamika kuwa kwa sasa Tanzania tunalojukwaa moja kubwa ambalo ni Swahili Fashion Week. Jukwaa ambalo linafanya kitu hiki hiki ambacho Afroswagga Fashion Awards inatarajia kukifanya.
Ingwa Swahili Fashion Week ni jukwaa kongwe lakini bado kuna changamoto ya kadhaa ikiwemo ya nafasi za ushiriki kuwa chache. Hili linatokana na ukuaji wa kasi wa tasnia hii ya mitindo na urembo nchini hasa baada ya kuja kwa internet na baadae mitandao ya kijamii. Swahili Fashion Week limebaki kuwa jukwaa kongwe na kila mwanamitindo ana ndoto ya kulifikia siku moja.
Hii ndio sababu ya Afroswagga kama blog ambayo bado changa na ambayo imezaliwa katika kizazi hiki cha internet na mitandao ya kijamii tumeona kuna haja ya kuja na jukwaa ambalo litatoa nafasi kwa wabunifu ambao kwa namna moja au nyingine wanakosa nafasi ya kupanda katika Swahili Fashion Week na majukwaa mengine.
Ieleweke kwamba hatushindani na Swahili Fashion Week. Wala hatusemi kama Swahili Fashion Week ni jukwaa la kichoyo au ni jukwaa baya, la hasha. Lakini kwa kuwa tasnia inakuwa kwa kasi, kila siku vinazaliwa vipaji vipya hivyo Swahili Fashion week peke yake haitatosha, ipo haja ya kuwa na majukwaa ya namna hii mengine mengi ili kukidhi mahitaji yaliyopo.
Mwaka huu 2018 Afroswagga Awards zimezaliwa, na kwa mwaka huu zitafanyika Mtandaoni tu ikiwa na vipengele 15, nisingependa kuzungumzia mwakani kwakuwa bado mipango inaendelea. Lakini tutatumia maoni ya watu katika kupata washindi ambao tutawatangaza kupita kurasa zetu za mitandao ya kijamii kadhalika na Blog yetu. Rai yangu kwa jamii ya fashion na urembo nchini, tujitokeze kupendekeza washindi wetu katika comments na Polls mbali mbali tutakazo ziweka kupita mitandao ya kijamii. Kama bado haujatufata katika kurasa zetu unaweza kufanya hivyo sasa hivi, Instagram ni @afroswagga, Twitter ni @afroswaggatz na Facebook ni @afroswagga
Mwisho kabisa tungependa kuwashukuru wadhamini wetu Darling Hair Tanzania na The Show Gamez kwa kutuamini na kuiweka mbele jamii ya Fashion nchini, tunathamini sana mchango wao katika hili, Bila kuwasahau #AfroMates kwasababu wao ndio hasa wamekuwa karibu nasi na kututia nguvu ya kuendelea mbele. Lakini hii sio tamati Afroswagga ikiwa kama blog ya watu ambayo inaendeshwa kwa mawazo ya wanajamii wa Fashion nchini kila mtu anakaribishwa kutoa mchango wake wowote alionao katika kujenga jamii bora na imara ya Fashion.
Kwa udhamini unaweza kuwasiliana nasi kupitia nambari: +255 712 578 838 au barua pepe: afroswggatz@gmail.com
Related posts
6 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Find More to that Topic: afroswagga.com/mitindo/afroswagga-fashion-awards/ […]
… [Trackback]
[…] Here you can find 42425 additional Information to that Topic: afroswagga.com/mitindo/afroswagga-fashion-awards/ […]
… [Trackback]
[…] Find More to that Topic: afroswagga.com/mitindo/afroswagga-fashion-awards/ […]
… [Trackback]
[…] Here you will find 85193 additional Info on that Topic: afroswagga.com/mitindo/afroswagga-fashion-awards/ […]
… [Trackback]
[…] Find More on on that Topic: afroswagga.com/mitindo/afroswagga-fashion-awards/ […]
… [Trackback]
[…] Read More on to that Topic: afroswagga.com/mitindo/afroswagga-fashion-awards/ […]