SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Aina 6 Za Mavazi Usipoteze Pesa Yako Kununua
Mitindo

Aina 6 Za Mavazi Usipoteze Pesa Yako Kununua 

Well dressed woman anaonekana yaani ukimuona tu unajua huyu dada anajua kuvaa, na hii inatokana na wao kujua nini wanunue,nini wasinunue, nini wavae na kitu gani na kipi hakiwafai. Ukiachana na kujua umbo lako ni muhimu pia kujua ni vitu gani si lazima kuwa navyo hata kama vinaendana na umbo lako.

Leo tunakuletea vitu vichache ambavyo huvihitaji na usimalize pesa yako kuvinunua.

  • Kununua Mavazi Kwasababu Umeona Influencers Wamevaa

Kuna makampuni ambayo wanalipa influencers wavae mavazi yao, kila kona unayopita unakutana na hilo vazi, ukalipenda na kuamua ulinunue na wewe hata kama unajua au unaona kabisa hili vazi hutolivaa huko mbeleni, hakikisha unajua ku-control matamanio na nunua vazi endapo tu utaona utalivaa mara nyingi, kabla ua kunua hilo vazi jiulize maswali haya.

  • Je nitalivaa hili vazi?
  • Je linaendana na life style yako?
  • Je linaendana na style zako nyingine za mavazi?

Kama maswali yote haya jibu lake ni hapana basi achana na vazi hilo.

  • Epuka Edgy Trend

Kuna trend ambazo zipo bold yaani zile ambazo ziko tofauti kwamfano kwasasa kuna trend ya patchwork denim, jeans ambazo zina viraka viraka, kwasasa kila unapopita unakutana na mtu amevaa na inaonekana sawa kwasababu ipo kwenye trend, lakini umejiuliza miezi kadhaa mbele utaweza kuvaa tena hili vazi pale ambapo trend itakuwa imeisha? Kama ungependa kufuata trend hakikisha unanunua kitu ambacho hata trend ikipotea kinaweza kuvalika.

  • Usinunue Mavazi On Sale Sababu Tu Yapo On Sale

Tunapenda ku-save pesa unakutana na vazi unaona bei rahisi basi unaamua kununua kuna neno wahenga walisema “bure aghari” kuna sababu ya kwanini iko kitu kipo onsale kwanini hakija uzika, hakikisha hata kama umekutana na vazi au accessory zipo kwenye sale zinaendana na style yako. Unanunua kitu sababu tu bei rahisi lakini mbeleni hukitumii hata kama ni pesa ndogo umetumia bado inakuwa haina maana.

  • Cheap Fabric

Hakuna kitu kina haribu muonekano kama cheap fabric, inawezekana umeona gauni zuri, style yako linakukaa vizuri mwilini lakini kama fabric yake ni mbaya achana nao, sio tu litakufanya uonekane cheap lakini pia linaweza kuharibika kwa urahisi.

Kununua Mavazi Yasiyo Endana Na Umbo Lako

Hiki ni muhimu sana unapoteza pesa unaponunua vazi ambalo haliendani na umbo lako, kwa maana hutolivaa na hata kama ukiwa kichwa ngumu ukavaa basi wengi watakuwa wanakushangaa na hautokuwa comfortable hakikisha unatumia pesa yako kwa kitu ambacho utavaa na kuwa comfortable nacho.

Kununua Fake

Inawezekana unapenda vitu vya brand fulani na hauna uwezo wa kununua, haimaanishi ununue fake yake, nunua kitu chenye quality hata kama sio brand kubwa lakini kiwe kizuri kuliko kupoteza pesa kwenye fake.

Related posts