SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Aina Tisa Za Viatu Hupaswi Kukosa Kuwa Navyo
PROV.145-9-2014
Mitindo

Aina Tisa Za Viatu Hupaswi Kukosa Kuwa Navyo 

Well unaweza kuwa na viatu vingi kwenye kabati lako kiasi ambacho una sahau vingine ni vya nini na wakati mwingine unakuta vimekaa tu kabatini wala huvivai unajiuliza ni kwanini umevinunua? kama ilivyo kwenye mavazi kwenye viatu pia kuna vile vya muhimu ambavyo hupaswi kukosa kuwa navyo kwa kuliona hilo our girl @style.with.mimie amekuletea viatu 9 ambavyo hupaswi kuvikosa katika kabati lako.

Aina 5 Za Viatu Kila Mwanadada Ana Paswa Kuwa Navyo

 

Stiletto nyeusi

Stilletto, hususani nyeusi ina uwezo wa kubadili muonekane wowote ule. Kiatu hiki huongeza vionjo na kufanya mvaaji aonekane kama amepangilia mavazi yake na pia hufanya mtu aonekane classic. Viatu hivi huendana na vazi lolote, unaweza valia tshirt, blauzi, koti, gauni refu au fupi. Kila kitu kinakaa.

Flat sandals

Hivi ni kwaajili ya siku unazotaka kupumzisha miguu kama wewe ni mtu wa kuvaa viatu virefu mara nyingi. Pia ni vizuri kwa safari  fupi na kuna baadhi ya mavazi na shughuli ambazo huitaji viatu simple vinavyokupa amani.

Simple yenye rangi inayoendana na nguo zako nyingi

Wengi tunaviita simple, ni viatu flat vya kufunika. Ni muhimu kuwa na pair ya simple. Simple pia huongeza umaridadi hasa kwa watu wasiopenda kuvaa viatu vyenye kisigino kirefu. Badala ya kuvaa sandals, ni bora kuvaa simple maana simple hufanya mtu aonekane kavaa casual zaidi. Unaweza vaa simple hata na suti, inategemea tu ni simple aina gani.

Mules aina yoyote

Hivi viatu vinatrend sana, viatu hivi ni vile vya kupachika mguu tu wakati wa kuvaa. Viko comfortable sana na vinavutia. Unaweza kuwa na mules fupi au zenye kisigino kirefu, maamuzi ni yako. Mules zitafanya uonekane chic and stylish endapo utavalia mavazi sahihi.

Boots

Kwa bahati mbaya sana, waafrika wengi huwa hawana muda wa kufuatilia majira. Kwenye mvua utatuona tunakimbizana na mwamvuli ila chini kuna sandals badala ya buti, kweli?? This is so not right. Kuna buti zimejaa tele kwa bei uitakayo. Buti huja kwa mitindo mbalimbali so unaweza chagua inayoendana na mitindo yako ya uvaaji. Wakati wa mvua buti husaidia sana ukizingati barabara uwa zinajaa maji kutoka kwenye vyanzo mbalimbali. Mbali na mvua, buti hupendezea zaidi kwenye baadhi ya mavazi na zipo nyingi tu zinazowzleza kuvaliwa kwenye nyakati mbalimbali.

High heel sandals

Viatu virefu kiasi vya wazi ni muhimu zaidi kwenye casual na smart casual looks. Hivi viatu viko simple sana ila vinaongeza unadhifu wa hali ya juu. Vinapendeza zaidi ukiwa umekata kucha vizuri na kupaka rangi. Miguu yako tu itaonyesha namna gani unajijari. Hakikisha vina mikanda imara na haviumizi wakati wa kutembelea. Ikibidi jaribu kuvitembelea kidogo dukani kabla hujanunua.

Raba

Raba zinakupa muonekano casual lakini bado unakuwa unaonekana umejipangilia kwenye suala zima la uvaaji. Pia hutaki kuvaa sandals au simple flats wakati wa mazoezi hivyo kuwa na raba inasaidia sana. Ukiwa na pair nzuri ya raba na ukiivaa na mavazi sahihi utapata muonekana flani mkali sana.

High heel yenye kisigino kinene.

Kuna siku unatamani kuvaa kiatu kirefu lakini hutaki zile stress za kubalance kiatu na maumivu. Kiatu kirefu chenye kisigino kinene uwa rahisi zaidi kutembelea maana kunatoa balance na support ya kutosha. Pia kwa watu ambao si wazoefu sana wa kuvaa michuchumio basi anza na viatu vya aina hii mpaka pale miguu itapozoea.

Viatu “Nude”

Viatu nude ni viatu vyenye rangi ya mwili wako. Yani rangi ya kiatu ikaribiane sana na rangi ya ngozi yako. Watu wengi wamekariri nude ni ile nude inayofanana na rangi ya ngozi ya mzungu ila hiyo sio kweli. Nude inaweza valika na rangi nyingine yoyote hivyo siku ukikosa kiatu kinachoendana na rangi ya nguo basi una uhakika wa kuvaa nguo hiyo na kiatu “nude”

kuwa na vyote hivi ni safari huitaji kuiharakisha kama huna pesa take your time kununua kimoja kimoja at a time.

Related posts

5 Comments

  1. magic mushroom chocolate bars

    … [Trackback]

    […] Find More Information here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/aina-tisa-za-viatu-hupaswi-kukosa-kuwa-navyo/ […]

  2. Where to buy magic mushroom online New South Wales

    … [Trackback]

    […] Read More to that Topic: afroswagga.com/mitindo/aina-tisa-za-viatu-hupaswi-kukosa-kuwa-navyo/ […]

  3. Sexy Baccarat

    … [Trackback]

    […] Find More Information here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/aina-tisa-za-viatu-hupaswi-kukosa-kuwa-navyo/ […]

  4. pg slot

    … [Trackback]

    […] Find More to that Topic: afroswagga.com/mitindo/aina-tisa-za-viatu-hupaswi-kukosa-kuwa-navyo/ […]

  5. stapelstein

    … [Trackback]

    […] There you will find 13143 additional Info to that Topic: afroswagga.com/mitindo/aina-tisa-za-viatu-hupaswi-kukosa-kuwa-navyo/ […]

Comments are closed.