SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Aina Za Tai Na Mavazi Yanayoendana Nazo
men fashion column

Aina Za Tai Na Mavazi Yanayoendana Nazo 

Kwa kijana ambaye hupenda unadhifu na kutaka kupendeza katika kila aina ya tukio basi hatoweza kuwa na tai chache katika kabati lake. Twaona tai mara nyingi zimezoeleka kuvaliwa maofisini na katika sherehe na kukaririwa tai lazima ivaLiwe na suti.

Well leo tutawaelezea aina za tai na wapi zavaliwa pia ni aina gani ya mavazi yaweza enadana na tai hiyo.

  • Necktie

Hizi ni tai ndefu zilizozoeleka kuvaliwa na suti maofisini, katika sherehe na matukio official. Styling tip katika kumatch tai hii na outfit yako ni kuwa makini katika kuchagua rangi na prints ili ziweze kuco-ordinate na rangi za outfit yako.

  • Skinny Necktie

Hizi ni tai ndefu lakini nyembamba. Hupendelewa na vijana maana zakufanya uonekane more fashionable na mwenye mwili mdogo. Waweza vaa ofisini, sherehe au on any formal ama casual event. Muhimu ni upangiliaji wa rangi na mavazi yako iwe wavaa suruali za kitambaa ama cadet au suti ya aina yoyote ile

  • Bow Tie

Tai fupi zivaliwazo shingoni ambapo uchaguzi wake wategemea na aina ya nguo uvaayo na eneo uendalo. Pindi uvaapo suti aina ya tuxedo basi yatakiwa uvae tai aina hii. Umakini wahitajika katika uchaguzi wa rangi kuepusha kujichanganya hivyo plain colours ni nzuri Zaidi. Ila pindi unapohudhria tukio kama sherehe au unapotoka out, waweza cheza na rangi pia patterns na dots kuupa muonekano wako uang’avu zaidi.

  • NeckerChief

Ni scarfs ambazo huvaliwa kwa kufungwa shingoni. Hizi ni more stylish and fun na waweza style pamoja na casual outfit yako pale unapotoka out on a fun occasion au red carpet. Itakutofautisha na kukupendezesha zaidi.

Imeandikwa na @willibard_jr

Related posts