SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Airport Looks From Wasafi Festival Performer’s
Mitindo

Airport Looks From Wasafi Festival Performer’s 

Kama kuna kitu tunakitupia macho kwasasa ni Wasafi festival, tunapenda kuona namna ambavyo wasanii wapo pamoja na kutupa ideas mbalimbali za mavazi. Ikiwa week hii festival hii inaelekea Sumbawanga tumeona wakiwa ndio wako safarini kuelekea sehemu husika tukaona sio mbaya kuleta hapa airport sytles zao na utuambie ya nani imekuvutia zaidi?

Diamond Platnumz, Darassa & Noel Gio wakiwa wamevalia hoodie na suruali wakiwa wamevalizia mionekano yao na miwani na accessories mbalimbali.

Mbosso, G Nako pamoja na Chegge hawa walichagua kuvaa jackets & sweater’s na suruali za jeans. Mbosso na Chegge walivalia kicks na kofia huku G nako yeye akiwa amechagua kuwa less kwa kutoku accessories na chochote bali attention yake alimalizia kwenye viatu aina ya boots zenye kisigino kirefu kidogo.

Tuliwaona Mzee Wa Bwax, Mr. Blue na J Melody wakiwa kwenye colorful looks ikiwa kila mmoja akiwa na style yake iliyompendeza kuvaa katika safari yake.

Alikuwepo pia Barnaba, Lil Ommy pamoja na Bill Nas, ambapo Barnaba yeye alikuwa amevalia t shirt nyekundu, jacket pamoja na suruali akamalizia na boots na accessories mbalimbali, Lil Ommy alikuwa na details mbalimbali kama kofia, scarf na miwani huku outfit yake ikiwa simple, Bill Nas yeye alichagua kuwa kwenye Denim on Denim amemalizia muonekano wake na kiccks, bandana na miwani.

Tuambie muonekano wa nani umekaa ki-airport zaidi kati ya hawa?

Related posts