Ally Rehmtullah ni moja kati ya wabunifu wakubwa wa mavazi hapa nchini Tanzania,ambaye amewahi kufanya aina nyingi za ubunifu wa mavazi pamoja na kushiriki katika matamasha makubwa ya ubunifu wa mavazi ndani na nje ya Tanzania.
Ni wiki moja imepita tangu kufanyika kwa onyesho la Sanaa Fashion lililofanyika kwenye ukumbi wa Mbezi Garden, Sanaa Fashion ambayo ililenga zaidi wabunifu chipukizi na kufanikisha hilo kwa kiasi kikubwa.
Miongoni mwa wabunifu walioshiriki katika onyesho la Sanaa Fashion ni Walter, Assia, Hameed,Jay Julius, Joyce collection, Benja Parfect, Kinen, Faima collection, Jacky Mandoza pamoja na Mgombelwa
Moja ya wabunifu chipukizi walionekana kufanya vizuri ni Mgombelwa kutoka Morogoro ambapo mavazi yake yalionekana ni yenye ubora wa hali ya juu, nakupelekea watazamaji walioko kwenye onyesho kushangilia kwa sauti za juu.
Sanaa Fashion iliudhuliwa na mastaa kama Martin Kadinda,Bob junior pamoja na Ally Rehmtullah, Akiongea na AfroSwagga Ally Rehmtullah alisema “Nawapongeza waandaji maana ni kitu kizuri kwa wabunifu chipukizi, Tanzania hakuna onyesho kama hili linalowapa nafasi wabunifu chipukizi. Nawapongeza tena waandaaji na hili lisiishie hapa ila iende mbele zaidi na zaidi ikibidi kila mwaka mara moja Alisema”
Related posts
3 Comments
Leave a Reply Cancel reply
You must be logged in to post a comment.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Find More here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/ally-rehmtullah-aipongeza-sanaa-fashion/ […]
… [Trackback]
[…] Read More on that Topic: afroswagga.com/mitindo/ally-rehmtullah-aipongeza-sanaa-fashion/ […]
… [Trackback]
[…] Read More on on that Topic: afroswagga.com/mitindo/ally-rehmtullah-aipongeza-sanaa-fashion/ […]