SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

BAIBUI VAZI LA STARA
Mitindo

BAIBUI VAZI LA STARA 

Faryz
Kila kunapokucha mambo yanazidi kubaadilika, teknolojia inazidi kukua , wigo wa Sanaa ya mitindo unazidi nchini Tanzania  na ulimwenguni kote kwani hakuna anaetaka kubaki nyuma katika  ulimwengu wa mitindo .
Wabunifu nao wanazidi kushika hatamu kwa kubuni vitu mbalimbali  ilimradi tu kuwafanya watu kuwa na muonekano  tafauti tofauti.
AfroSwagga imefanya mahojiano  na mmoja wa wabunifu wa mabaibui nchini Tanzania anaejuliakana kwa jina  la Faryz nae alikua na haya ya kusema

AfroSwagga : Unauzungumziaje ulimwengu wa mitindo Tanzania?
Faryz: Kiukweli mitindo inazidi kupanuka kila siku  kadri teknolojia inavyokua watu wanazidi kuelewa,  kupenda  na kujua umuhimu wamitindo katika maisha .

AfroSwagga : Kwanini uliamua kubuni mabaibui na sio kitu kingine?
Faryz: Sababu kubwa  niliona vazi la baibui limechukuliwa kama vazi la msimu mfano wakati wa ramadhani  lakini sivyo ivo baibui ni vazi unaloweza kuvaa mahali popote na wakati wowote, kwani ni vazi la stara linalokufanya kuwa huru mahali popote.

AfroSwagga : Wabunifu wengi wanabuni vitu kwa kuwalenga vijana Zaidi ni kwanini na kwanini  wewe unaona  uko tofauti?
Faryz: Kitu kikubwa ambacho wengi wanaangalia ni soko, vijana ndio kundi kubwa la watu wanaopenda kwenda na mitindo kuliko watu wengine  ndio maana wengi wanawaangalia vijana Zaidi lakini mimi niko tofauti kwani baibui halichagui umri mtu yoyote anaweza kuvaa baibui.

AfroSwagga: Changamoto gani ambazo unakutana nazo katika kazi yako ya ubunifu?
Faryz : Changamoto kubwa ambayo nakutana nayo mimi kama mimi ni ukosefu wa malighafi hapa nchini , kwani mimi natumia mabaibui ya mitumba nabuni tofauti lakini watu wanayapenda,

AfroSwagga: Onesho la Mitindo liliyofanyika jumamosi ya tar13 ( stara)lengo la kuandaa onesho hilo lilikua ni nini, na kwanini mkaipa jina la stara?
Faryz : kwanza sababu iliyofanya  tuipe jina na  stara ni kwa sababu baibui ni vazi la stara na lengo la onesho ilikua ni kuwakumbusha watu hasa wanawake kujistiri sio kipindi tu cha ramadhani ila muda wote watu wakumbuke kujistiri

AfroSwagga : unatoa ushauri gani kwa wabunifu wadogo  ambao wanatamani kufanya kazi hii lakini hawajui wapi pa kuanzia
Faryz: Kitu chakuzingatia nikujiamini na kuipenda kazi yako, pia watumie mitandao ya kijamii kujitangaza watafika mbali na kutimiza malengo yao , mimi ni mitandao ya kijamii iliyonisaidia kujitangaza na kutangaza kazi yangu.

AfroSwagga: Unatoa ushauri gani kwa jamii
Faryz:  Jamii ichukulie mitindo kama sehemu ya maisha na   pia  wasiruhusu mitindo kuharibu mila na desturi za Tanzania nawasihi sana wanawake wakumbuke kujistiri ili kujilindia heshima katika jamii.

 

JIONEE UBUNIFU WAKE KATIKA PICHA

IMG-20150614-WA0032IMG-20150614-WA0030IMG-20150614-WA0031IMG-20150614-WA0036

IMG-20150614-WA0023    IMG-20150614-WA0034


Kwa Picha zaidi unaweza kutembelea ukurasa wake wa Instagram @my_hijjab_my_stara

Related posts

2 Comments

  1. review

    … [Trackback]

    […] Find More Information here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/baibui-vazi-la-stara/ […]

  2. shroomies edibles

    … [Trackback]

    […] There you can find 98794 additional Info to that Topic: afroswagga.com/mitindo/baibui-vazi-la-stara/ […]

Leave a Reply