SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Balozi wa Italia atakuwa wenyeji wa SFW Pop-Up shop nyumbani kwake Juni 2 2018
Mitindo

Balozi wa Italia atakuwa wenyeji wa SFW Pop-Up shop nyumbani kwake Juni 2 2018 

Habari Njema! Balozi wa Italia nchini Tanzania, kwa mara nyingine tena atakuwa wenyeji wa onesho hili la Swahili Fashion Week Pop Up shop litakalo fanyika tarehe 2 mwezi juni kuanzia saa sita mchana hadi kumi na mbili jioni, ni sehemu pekee utakayopata nguo na vito  vya hali ya juu kutoka kwa wabunifu mashughuli watakao simamia uuzaaji wa bidhaa zao bora.

Onyesho hili la siku moja lenye lengo la kuonesha bidhaa mbalimbali  zinazotengenezwa kwa mkono kutoka kwa wabunifu wa ndani na nje ya nchi pamoja na wasanii wa uchoraji kutoka sehemu tofauti nchini Tanzania watakuwepo nyumbani kwa balozi wa Italia  eneo la Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Onesho hili la pop up shop linawapa nafasi wafanyabiashara na wajasiriamali kuuza bidhaa zao kwa jamii ya kidiplomasia na watu wengine tofauti, pia litawakutanisha na wabunifu wa nguo, wabunifu wa vito, watengeneza mapambo ya ndani, na wasanii wa uchoraji.

Waandaaji wa Onyesho hili wanawasihii wajasiriamali wa kitanzania wanaokuza bidhaa “zinazotengenezwa Tanzania” kuchukua nafasi hii kukuza mtandao wakibiashara na kuongeza wateja na kupata nafasi ya kushiriki kwenye maonesho  ya Swahili Fashion Week Bazaar yatakayo fanyika mwezi Disemba mwaka huu. Onesho hili lina jumla ya washiriki 40, baadhi yao ni, Jamilla Vera Swai, MM Collection, Xarafa, Neste Fashion Africa, Kiwohede, Naledi Tanzania, Lulua Gems, Diana Quilt and Designs, ABLO, Yasmar Perfumes, Kekuune, Hucna designs, Zawadi Zanzibari na wengine wengi.

Onyesho la SFW Pop Up shop linawakaribisha watu wote wafike nyumbani kwa balozi wa Italia, oysterbay, jumamosi ya tarehe 2 mwezi juni, hakuna kiingilio , vinywaji vitakuwepo na utapata nafasi ya kununua bidhaa mbalimbali kutoka kwa waoneshaji.

Swahili Fashion Week Pop Up shop imeandaliwa na kampuni ya mawasiliano na uratibu matukio, 361 Degrees Africa kwa kushirikiana na Balozi wa Italia nchini Tanzania Mh. Roberto Mengoni

Kwa taarifa Zaidi na jinsi ya kushiriki tembelea tovuti yetu

www.swahilifashionweek.com au piga simu 0769 696 633/0713 844 48

Related posts

6 Comments

  1. psychedelic mushroom chocolate bars legal near north carolina

    … [Trackback]

    […] Read More on to that Topic: afroswagga.com/mitindo/balozi-wa-italia-atakuwa-wenyeji-wa-sfw-pop-up-shop-nyumbani-kwake-juni-2-2018/ […]

  2. Best magic mushroom shop New South Wales

    … [Trackback]

    […] Here you can find 87227 more Info to that Topic: afroswagga.com/mitindo/balozi-wa-italia-atakuwa-wenyeji-wa-sfw-pop-up-shop-nyumbani-kwake-juni-2-2018/ […]

  3. 토렌트 사이트

    … [Trackback]

    […] Read More Information here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/balozi-wa-italia-atakuwa-wenyeji-wa-sfw-pop-up-shop-nyumbani-kwake-juni-2-2018/ […]

  4. Buy DMT powder Belgium,

    … [Trackback]

    […] Find More to that Topic: afroswagga.com/mitindo/balozi-wa-italia-atakuwa-wenyeji-wa-sfw-pop-up-shop-nyumbani-kwake-juni-2-2018/ […]

  5. her comment is here

    … [Trackback]

    […] Find More here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/balozi-wa-italia-atakuwa-wenyeji-wa-sfw-pop-up-shop-nyumbani-kwake-juni-2-2018/ […]

  6. ARCADIA GAMING สล็อตออนไลน์ เว็บตรง อันดับ 1

    … [Trackback]

    […] Read More on on that Topic: afroswagga.com/mitindo/balozi-wa-italia-atakuwa-wenyeji-wa-sfw-pop-up-shop-nyumbani-kwake-juni-2-2018/ […]

Comments are closed.