SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Barua Ya Kufunga Na Kufungua Mwaka Kwa Wapenzi Wa Afroswagga
Mitindo

Barua Ya Kufunga Na Kufungua Mwaka Kwa Wapenzi Wa Afroswagga 

2019 tumeshuhudia ukuaji katika tasnia ya urembo, mitindo na ubunifu, muziki yaani sanaa kiujumla. Ubunifu katika kazi za wasanii wengi, uwepo wa talents toka  kwa vijana wanaochipukia katika sekta mbalimbali iwe styling, photography, make up artistry, modelling pia fashion designing.

Lengo kuu la Afroswagga sio kukosoa siku zote bali kuonyesha wapi ni sawa na wapi tunakosea ili kuweza boresha mapungufu pale yanapoonekana. Pia twafurahia kuona vijana wadogo na chipukizi wakijitokeza na kuonyesha kazi zao.

Mifano iliyo hai ya vijana waliothubutu katika baadhi ya Sekta ni pamoja na Vaazi, Howard Son, Macrida Joseph katika styling. Nasra, Eddie, Zuhuraty katika make up artistry. Pia tasnia ya mitindo tuliweza onyesho kubwa la mavazi, Swahili Fashion Week likiwapa nafasi models chipukizi

Hakika Tanzania ina vipaji vingi toka kwa vijana na hii yatupa faraja pale tunaipoitazama miaka ya baadaye. Hatuwezi taja chipukizi wote  maana ni wengi lakini kazi zao zaonekana na zatupa matumaini ya kukua kwa tasnia ya ubunifu, mitindo na ubunifu.

2020 ombi letu ni kwa wakongwe katika tasnia kuweza kuwapa nafasi vijana kuweza onyesha kazi zao kwa jamii. Hii ni rai kwa wasanii, watengeneza filamu, mastaa nchini na wadau wote wa tasnia ya sanaa kwa ujumla.

Na kwako kijana nyumbani, mtaani mwenye kipaji iwe ni ubunifu wa mavazi na accessories , upigaji picha, styling, make up au modelling, usiogope bali anza sasa, wote uwaonao  wakifanya vizuri walianzia chini. Afroswagga ipo wazi kwa ushauri na uelekezi siku zote maana twaamini katika ukuzaji wa vipaji. Our DMs, e-mails pia namba za simu zipo wapi. 

2020 twarajia kuona talents mpya na nyingi zitakazoiinua nchi yetu kimataifa. Twawatakia heri ya mwaka mpya 2020 Afromates.

Yours truly, 

Afroswagga.

Related posts

3 Comments

 1. เว็บพนัน

  … [Trackback]

  […] Information to that Topic: afroswagga.com/mitindo/barua-ya-kufunga-na-kufungua-mwaka-kwa-wapenzi-wa-afroswagga-2/ […]

 2. ecstasy drug movie,

  … [Trackback]

  […] Find More to that Topic: afroswagga.com/mitindo/barua-ya-kufunga-na-kufungua-mwaka-kwa-wapenzi-wa-afroswagga-2/ […]

 3. vegan mushroom soup recipe​

  … [Trackback]

  […] Find More on on that Topic: afroswagga.com/mitindo/barua-ya-kufunga-na-kufungua-mwaka-kwa-wapenzi-wa-afroswagga-2/ […]

Comments are closed.