SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Barua Ya Kufunga Na Kufungua Mwaka Kwa Wapenzi Wa Afroswagga
Mitindo

Barua Ya Kufunga Na Kufungua Mwaka Kwa Wapenzi Wa Afroswagga 

Mwaka 2018 umeweza kuwa wa mafanikio makubwa mabapo tumeona tasnia ya urembo, mitindo na ubunifu ikizidi sogea mbele. Twaweza sema hapa tulipo  si sawa na miaka 5 nyuma na hakika tujipongeze kwa hili.

Tasnia ya urembo, mitindo na ubunifu yawakutanisha watu wengi wakiwemo wabunifu wa mavazi, make-up artists, photographers, stylists, models, bloggers, style influencers, wanasanii iwe muziki ama filamu na wengine wengi. Kila mmoja hapa ana mchango wake nasi Afroswagga tungependa kutoa rai kwa ila muhusika.

  • Wasanii

Hasa katika tasnia ya muziki ambayo inakuwa kwa kasi sana na kuangaliwa sana na mataifa mbalimbali, tungependa kuona wabunifu nchini wakitumiwa katika kazi zenu kwa wingi. Wasanii wengi wakipendelea kuvaa mavazi toka nje na mengi yakiwa feki huku kuna wabunifu nchini ambao wangeweza fanya zaidi katika kazi zao.

KUNA UMUHIMU WA WASANII KUWA NA WABUNIFU WAO?

  • Stylist

Tulizungumzia wasanii kuwatumia stylists katika kazi zao na hiki tumeona wengi wakilifanyia kazi lakini pale stylists wanapotumika hatuoni tofauti na wengi wao huendelea kuwavalisha wasanii nguo zile zile, creativity na style personality inakosekana, tungependa mwaka huu tuone tofauti tupate ladha tofauti hii italeta ushindani na chachu ya stylist kufikiria wafanye nini kutoka nje ya box na kuwafanya watu maarufu wawe na mionekano ya kipekee na mizuri.

BADO TUNAHITAJI MA STYLIST KATIKA VIDEO SHOOTING

  • Style Influencers

Fashionstas wengi nchini wana uwezo wa kuwainspire Watanzania wengi katika suala la mavazi. Wengi wetu, ambao tumhepedeza pendeza pia twaishia kulike tu picha. Tutapendelea tukiona watanzania wengi wakipendezwa na kukoshwa na kazi za style and fashion influencers wetu ambapo mtanzania wa kawaida naye aweze ona na kusema name naweza pendeza kama fulani akitumia nguo zake ziwe mtumba ama dukani, lakini pia kutoa tips now and then ili wa Tanzania wapate kujifunza kutoka kwenu pia, lets make Tanzania Fashionable.

  • Wabunifu

Hakika twaendelea jivunia wabunifu wengi wakubwa kwa wachanga tulionao katik fani hii. Ni kazi nzuri yafanyika. Lakini twaomba kwa wachache wanaokosea kujirekebisha hasa katika crearivity maana wengi walalamikiwa kuwa sio wabunifu bali wacopy mishono toka nchi nyingine. Tungependa kuona Made In Tanzania kweli ambapo hata mastaa toka nchi nyingine wataweza vaa kazi zenu. Creativity ianzie toka uchaguzi wa materials and fabrics, designs, mishono, finishing na hata adveristing of the brand.

Tunatengeneza Aina Gani Ya Kizazi Cha Wabunifu Wa Baadae?

  • Photographers Na Makeup Artist

Kazi nzuri sana yafanywa na makeup artists na wapicha picha wakishirikiana na wabunifu lakini pale kitu chochote kinapozidi, hupoteza uhalisia. Edits za kupita kiasi hadi nguo na ngozi ikibadilika tuache hizi mambo. Pia makeup zisizoendana na tukio nazo twaomba zibaki 2018.

2018 ilikuwa nzuri, 2019 tuipaishe bendera ya nchi yetu kupitia fashion & beauty mbali zaidi.

Related posts

4 Comments

  1. hk usp expert.45

    … [Trackback]

    […] Here you will find 39888 more Info to that Topic: afroswagga.com/mitindo/barua-ya-kufunga-na-kufungua-mwaka-kwa-wapenzi-wa-afroswagga/ […]

  2. ephedra sinica tea for sale

    … [Trackback]

    […] Read More here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/barua-ya-kufunga-na-kufungua-mwaka-kwa-wapenzi-wa-afroswagga/ […]

  3. dmt vape cartridge for sale​

    … [Trackback]

    […] Read More Info here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/barua-ya-kufunga-na-kufungua-mwaka-kwa-wapenzi-wa-afroswagga/ […]

  4. Click On this site

    … [Trackback]

    […] Read More on that Topic: afroswagga.com/mitindo/barua-ya-kufunga-na-kufungua-mwaka-kwa-wapenzi-wa-afroswagga/ […]

Comments are closed.