SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Behind The Brand: Just MK By Martin Kadinda
Mitindo

Behind The Brand: Just MK By Martin Kadinda 

Leo nyuma ya brand tuko nae Martin Kadinda, huwezi kutaja Tasnia ya Mitindo na Ubunifu Tanzania na usimtaje Martin. Tunaweza kusema Martin amekuwa na Industry au Industry imekuwa na Martin, ameanza ubunifu akiwa mdogo na mpaka sasa huwezi acha kumtaja katika 10 bora ya wabunifu Tanzania.

Ukiachana na uwezo wake mkubwa kwenye ubunifu, Martin ni kati ya wale wabunifu wanaojipenda na kuvaa vyema katika maisha yao ya uhalisia, iwe casual au akiwa kwenye matukio maalum.

Kwenye casual huwa anatafuta namna ya kufanya muonekano wake uwe casual ila classy kwa kumix casual clothes na classy, kama atavaa suruali ya kitambaa basi atavalia na t-shirt na raba, kama atavaa jeans basi atavalia shirt na moccasin, anajua nini afanye kunyanyua muonekano wake.

Akiwa kwenye matukio maalum ndio utapenda zaidi maana anajua ku-keep it classy & fashionable, chaguzi zake za rangi za mitoko yake pamoja namna ambavyo anakuwa less but more ndio kinacho mfanya awe tofauti zaidi.

sisi yetu ni hayo tu tuambie kwako muonekano upi wa Martin umeupenda zaidi.

Related posts