SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Bijoux Trend Celebrates Culture In Her 2021 Campaign
Mitindo

Bijoux Trend Celebrates Culture In Her 2021 Campaign 

We love when a designer steps outside the box, mara nyingi wabunifu wakitoa collection zao hawajisumbui kufanya vitu vingine kuendelea kutangaza collection zao hizo. Fashion Campaign ni namna mojawapo ambayo inamuwezesha mbunifu kutangaza collection yake, zipo namna mbalimbali za kufanya campaign hizi, kwa kuchagua aina gani ya watu ungependa kuwagusa na bidhaa yako kupita campaign yako hio.

Bijoux yeye amechagua kusheherekea utamaduni, Bijoux na team yake walisafiri mpaka singida & bagamoyo ku-shoot hii campaign ( the effort). Tumependa kwamba ameweza kuonyesha sio tu wadada na wamama wa mjini wanaweza kuvaa hizi nguo bali hata wale ambapo wapo vijijini wanaweza kuvaa. Na kwamba mavazi yake anayotengeneza yanaweza kuvaliwa na yoyote.

Bijoux hakwenda na models Singida bali walitumia watu wa kawaida, kwa mujibu wa Bijoux models wake hawa walikuwa ni baadhi ya ndugu wa stylist Vaazi ambae ndiye alikuwa art director kwenye campaign hio.

Lakini pia tumependa kwamba hawakwenda sehemu fancy sio kama vile ambavyo tumezoea kuona photo shoots nyingi zikifanyika, walienda kijijini na walionyesha mavazi yakiwa yamevaliwa nyumbani huku models hawa wakiwa wanafanya shughuli zao za kawaida kama kusukana, kusuka ukili, kutwanga etc.

Hii campaign imebeba uhalisia wetu na utamaduni wetu, tumependa tulichokiona na tunatamani kuona zaidi ya hivi kwa wabunifu wengine.

Art director #vaazi_stylist
Designer #bijou
Sniper #Kevoo
Location #bagamoyo / #Singida 

Related posts