SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Black Royal Excellence Ndio Theme Ya Outfit Zilizopo Katika Teaser Ya Wasafi Tv Reality Show
Mitindo

Black Royal Excellence Ndio Theme Ya Outfit Zilizopo Katika Teaser Ya Wasafi Tv Reality Show 

Familia ya mwanamuziki Diamond Platnumz ndio familia ambayo inaongoza kwa kufuatiliwa kwa sasa Africa Mashariki na hii inatokana na visanga vyao vya kila siku, kwa kuliona hilo wenyewe wameamua kukuleta maisha yao karibu na wewe, Well wametoa Teaser ya reality show yao ambayo inaitwa ” The  Real Life Of Wasafi (TRLOW)”

Kwetu tulikuwa tunasubiria teaser itoke kwa maana teaser ndio hubeba kila kitu kama itakupa hamasa ya kuangalia au lah, kwenye teaser hii tumeangalia sana outfit zilizopo nini kilikuwa nyuma ya hizi outfits tumemuuliza stylist wa Teaser hii ambae ni Noel Ndale amesema theme ilikuwa “BLACK ROYAL EXCELLENCE”

Tulivyo iona hii teaser kwa mara ya kwanza haraka haraka ikatujia image ya Coming To America, kwa wanaume suit walizo vaa na namna wame zi-accessorize kichwani ikatujia taswira ya movie ya Coming To America ya Eddie Murphy ambayo ilitoka mwaka 1988,

ukimuangalia Malomboso na Lavalava walivyo valishwa utaelewa tunaongelea nini

Esma yeye amepewa mavazi ya miaka ya miaka ya 1940 – 1960 ambapo wanawake walikuwa wanavaa magauni ya cinderella na gloves mikononi ilikuwa ni wanawake wachache sana wa ki-Africa ambao wanavalishwa hivi hasa wale wenye hadhi fulani katika jamii, lakini pia walikuwa wakivaa kwenye sherehe.

Kwa Queen Darleen, Diamond na walio baki style zao zipo kisasa zaidi, sana sana walicho ongezewa ni accessories ambazo zimekaa ni “royal”.

Tumependa fashion namna wamejaribu kufanya ionekane tofauti na teaser nyingine, lakini tungefurahi zaidi kama kungekuwa na fusion, yaani kuchanganya theme lakini zote zika blend in na sio kila moja kusimama kivyake, kama ambavyo unaona ukiwakeka Mboso na Lavalava unapata kitu cha tofauti, Diamond na Mose wakisimama wanaleta theme nyingine, Esma peke yake, mama Diamond, Romy, Harmonize Na Rayvanny wana theme nyingine.

All in all wamejaribu na we cant wait kuona nini kinakuja.

 

Related posts