SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Blogger Feature: Fashion & Beauty Talk With Maryam “Missie Popular”
Mitindo

Blogger Feature: Fashion & Beauty Talk With Maryam “Missie Popular” 

Anaitwa Maryma wengi tunamjua kama Missie Popular, ni Fashion Blogger kutoka hapa hapa Nchini kwetu. Ni moja kati ya ma-blogger wakubwa Tanzania hata sisi wakati tunaanzisha Afroswagga na mpaka sasa bado tunamuangalia, ameanzisha blog yake ya Missie Popular mwaka 2011 ina maanisha ana miaka 6 mpaka sasa tangu aanze hii kazi na bado jina lake lipo pale pale,sisi tunamuita “muhenga” katika swala zima la blogging Tanzania. Tume mtafuta hili kupata na kujifunza mawili matatu kutoka kwake

Afroswagga – Fashion ina maanisha nini kwako?

Missie Popular – Interest ya kufuata trends zinazoingia kila msimu. Fashion kwangu sio jambo muhimu kama kufahamu na kutengeneza STYLE yako inayokutambulisha wewe.

Afroswagga -Wewe ni Fashion Blogger, Na watu wanaamini fashion bloggers wanajua mitindo,kuvaa etc kwanini uliamua kujiita mshamba? au kufanya vlog ya mshamba

Missie Popular – Naamini kila mtu ana USHAMBA flani ndani yake,huwezi kujua kila kitu. Binafsi niligundua kuwa naweza kuwavalisha watu kama stylist lakini bado sijajifahamu mimi binafsi na style ninayoipenda Zaidi. Hapo ndipo MSHAMBA 101 idea ilipoanzia,ikiwa ni namna ya mimi mwenyewe kujifunza mambo mbalimbali na kuweza kuamua kile ninachotaka kuStick nacho kama style yangu. Bado Najifunza

 

Afroswagga – Tumeona mionekano yako mipya je hivi ndivyo utakavyo kuwa unaonekana siku zijazo?

Missie Popular – Hapana. Nitakua nafanya photoshoot mbalimbali zinazohusu designers,stylists na makeup artists tofauti ili kuangalia muonekano gani nimeupenda Zaidi na unaendana na mimi Zaidi. Kwahiyo picha hizi ni mwanzo tu wa safari ndefu ya kujitambua kama Fashion na Lifestyle blogger

Afroswagga – Umeamua kubadilika kwa ajili yako au kwa sababu ya kuitwa mshamba? 

Missie Popular – Mwaka 2011 nilipoanzisha www.missiepopular.blogspot.com sababu mojawapo ilikua kujifunza Zaidi kuhusu fashion industry ya Tanzania na dunia kwa ujumla. Miaka 6 baadae,naamini najua vingi sana lakini bado kuna kuExperiment ambapo sijafanya…Hivyo hii ni hatua ya pili. Kuhusu Kubadilika,hahahah nadhani nina sura Zaidi ya moja,nikiwa mtumishi wa Umma ni tofauti kabisa na tukikutana kama Missie Popular 😊

 

 

Afroswagga – Kama ungepewa nafasi ya kuchagua kabati la mtu yoyote maarufu ungechagua kuchukua kabati la nani? kwanini?

Missie Popular – Michelle Obama! Kabati lake ni aina ya kabati ninaloanza kulitengeneza,kabati litakaloniruhusu kusimama kama mtumishi wa Umma lakini wakati huohuo nikaonesha upendo wangu na interest kwenye fashion,hususani kwa kutumia wabunifu mbalimbali wa Afrika.

Afroswagga – nini kilikuwa kigumu kwako wakati una fanya photoshoot na Irfan katika muonekano wako mpya.

Missie Popular – Team iliyofanya photoshoot hii ilikua tofauti sana, na ukiacha Irfaan,wengine wote ni aina ya watu tunaofanana sana kimtazamo. Photographer Ally Zoeb, Designer Jamillah Vera Swai, Makeup Artist Rahima wa Simply Gorgeous na Accessories za Manyatta, wote ni watu ambao wanafanya mambo mengi na makubwa sana kwenye tasnia hii lakini brand zao ndio kubwa kuliko wao. Hii inasababisha tunapokutana tunakua karibu sana kama marafiki na Hakuna intimidation ya majina makubwa ama personalities. Sasa ukimwongezea Irfaan ndio kama catalyst wa kuchangamsha kila kitu kiasi kwamba mambo yanakua NATURAL. Hakukua na ugumu wowote maana Irfaan alikua anajua muonekano anaotaka na kila mtu akajipanga kufikia lengo…mapozi yakawa yanatiririka tu

Afroswagga – Upo kiasili (natural) kuanzia ngozi hadi nywele unaweza kutuambia tips unazo tumia kufanya ngozi yako iwe nyororo lakini asili na tip yoyote muhimu kwa natural hair

Missie Popular – Kula vizuri,kunywa maji mengi na jitahidi kulala masaa angalau 6 kwa siku. Ukiacha hivyo,mimi nafanya skin routine kila asubuhi na jioni kwa kutumia bidhaa za Oriflame ambazo ni natural. Kwenye nywele najaribu sana kukwepa matumizi ya moto (blow dry,pasi), na badala yake natumia Zaidi asali,aloe vera na parachichi kama conditioner na kuacha nywele zikauke naturally. Mafuta ya nazi nachanganya na black caster ndio ninayopaka kwenye nywele. Cha muhimu ni kutumia bidhaa za asili na kukwepa matumizi mengi ya moto kwenye nywele

Afroswagga – Tutajie fashion trend ambayo huwezi kuijaribu hata siku moja

Missie Popular – Color Block…I hope haitarudi tena kwenye fashion trends,ever!

Afroswagga – kama tukichungulia kwenye handbag yako tutakuta nini?

Missie Popular – 5 different shades of lipstic 😊 Napenda sana lipstic. Lazima utakua novel/book,notebook ya Lavy,pen, wallet, bubblegum, SD card ya camera, miwani, hand lotion na external drive

Afroswagga –  Kama fashion ambassador unajisikiaje ukiona msanii mkubwa ame haribu kuvaa katika mavazi?

Missie Popular – Nafurahi kanipa cha kuongelea kwenye blog…hahahaha. Am kidding! Zamani nilikua sielewi kabisaaaa maana naamini kama msanii mkubwa unatakiwa kuwa na team inayohakikisha unaonekana presentable mbele za watu….ila siku hizi nimeelewa namna tasnia ya Sanaa inavyoendeshwa kisanii,sishangai tena….ila its too sad maana kuna fursa nyingi sana zinatupita kwa kutokua professional na tasnia hii

Afroswagga – Tip 3 muhimu za kumwambia msomaji ambazo anaweza kufanya aonekane stylish kila siku.

Missie Popular – Vaa nguo za basic colors kama nyeupe,blue bahari n.k maana zinakufanya uonekane msafi na expensive Zaidi (nimejifunza hivi karibuni)… Pia viatu mchongoko (pointy shoes) kwa wanawake ziko stylish sana…Cha tatu, Nywele. Muonekano wa nywele unaweza kukufanya uonekane stylish ndani ya nguo za bukubuku,ama uonekne kituko ndani ya designer suite….hapa hata mimi bado najifunza Zaidi 😊

Afroswagga – Kama Fashion Blogger ambae upo kwenye industry siku nyingi unawaambia nini fashion bloggers wanao chipukia na watanzania kiujumla? 

Missie Popular – Kuweni ORIGINAL! Hamna mtu anataka kusoma blog yako na kukutana na mwandiko unaofanana na Shamim au Missie Popular, kaa chini uisikilize sauti yako na kuandika namna ambavyo WEWE unaamini na sio kile kila mtu anachoandika.

Pia,hii kazi inahitaji muda wako na umakini sana ili uweze kupata wasomaji wanaorudi kwako kila siku. Jitengenezee ratiba ya kupost na uifuatilie. Lakini usisahau kuwa,Instagram imeshageuka blog ya kila mtu,story zako jitahidi ziwe za kipekee ambazo siwezi kuzipata Insta.

Asante Missie Popular, tumejifunza mengi kupitia hii Interview kwa ambao mngependa kutembalea bloga yake hii hapa Missie popular, Kumfollow Instagram @missiepopular lakini pia kusoma interviews za wengine bonyeza hapa, Liliane Masuka, Lehautestyle, Natural Hair Tanzania, Nuya Essence

 

Related posts

5 Comments

 1. แทงบอลออนไลน์

  … [Trackback]

  […] Read More to that Topic: afroswagga.com/mitindo/blogger-feature-fashion-beauty-talk-with-maryam-missie-popular/ […]

 2. Buy DMT online Perth

  … [Trackback]

  […] Read More to that Topic: afroswagga.com/mitindo/blogger-feature-fashion-beauty-talk-with-maryam-missie-popular/ […]

 3. wapjig.com

  … [Trackback]

  […] Read More on on that Topic: afroswagga.com/mitindo/blogger-feature-fashion-beauty-talk-with-maryam-missie-popular/ […]

 4. toronto weed delivery

  … [Trackback]

  […] Information on that Topic: afroswagga.com/mitindo/blogger-feature-fashion-beauty-talk-with-maryam-missie-popular/ […]

 5. Bubble Tea

  … [Trackback]

  […] Information to that Topic: afroswagga.com/mitindo/blogger-feature-fashion-beauty-talk-with-maryam-missie-popular/ […]

Leave a Reply