SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Bongo Movie Na Fashion
Mitindo

Bongo Movie Na Fashion 

Huwa tunachukua muda kukosoa tunapoona makosa lakini pia huwa hatuachi kusifia pale panapo stahiki sifa, Miaka michache nyuma tulishawahi kukosoa bongo movies kutokana na makosa mbalimbali ya fashion leo tupo hapa kutoa pongezi kwao.

Hatujui kama walisoma au ni kwenda na wakati kwasasa bongo movies wanajitahidi sana katika swala la mitindo, wanavaa kutokana na sehemu walipo, tunapenda kuona kwenye sherehe wanavaa kama sherehe, kazini wanavaa kama kazini tumepiga hatua kutoka pale ambapo tulikua.

Makeup na nywele, kukumbuka tu nywele na makeup za miaka ya nyuma utaona namna ambavyo kuna tofauti sana sana kwasasa wengi wanajitahidi kupaka makeup nzuri na kusuka nywele zenye kupendeza.

Tumependa kwamba sasa hivi wanatilia mkazo mionekano yao kwenye movies na hivi ndivyo tunatakiwa kuwa na kupiga hatua zaidi, kuona tumeacha kuvaa kama vikatuni inatia moyo zamani ilikuwa vazi la club unakuta actress kavaa kazini, nywele imesimama ina rangi ya kazini mdada kasuka na ndio reception wa ofisini au makeup ya kwendea harusini yupo ofisini.

Sasa hivi tunaona mavazi, nywele, viatu unaenda na uhusika na mahali alipo muigizaji, tunapenda namna ambavyo mnawekeza katika swala la mionekano, Tuendelee hivihivi ata movies zetu zikionyeshwa nje wajue tupo serious.

Related posts