Kama wewe ni mpenzi wa Mitindo basi nina hakika umeshawahi kusikia hili jina CARA DELEVINGNE, ni msichana mdogo tu alie zaliwa mwaka 1992, Lakini jina lake ni kubwa katika ulimwengu wa mitindo
CARA DELEVINGNE ni mwana mitindo ambae amesha wahi kufanya kazi na wabunifu wakubwa kama Zara, Channel, H&M, British Vogue, Givenchy Na wengine wengi. Lakini kwa sasa mwana dada huyu ameamua kujikita Zaidi katika uigizaji wa Filamu hapa sasa tukapatwa na wasiwasi na maswali JE CARA DELEVINGNE ATAACHA MITINDO?
“siachi kazi yangu ya uanamitindo, wala sistaafu. Nafanya filamu kwa muda. Msichana huyu wa miaka 22 aliwaambia The Hollywood Reporter. “Kazi zinakua Na Unaendelea na Umri Unaongezeka Kuwa mzee. Bado nina mahusiano mazuri na watu niliokua nafanya nao kazi awali. Labda nitafanya mitindo nyakati nyingine, lakini kwa wakati huu sina muda wa kufanya chochote.
CARA DELEVINGNE ambae ame pokelewa kwa mikono miwili na waandishi wa filamu na wakurugenzi kwa kipaji chake na dhamira yake mpya, pia ana mashabiki wengi katika ulimwengu wa Mitindo, pia ana nia ya kukumbuka michango yao katika kazi yake ya awali hasa baba yake wa ubatizo katika mitindo bwana Karl Lagerfeld.
“Alikua akijua kwamba nataka kuigiza. Alikua sawa kuniingiza katika filamu yake ya mitindo” aliongeza “pia alijua kwamba nataka kufanya mziki, akaniacha nifanye mziki pia. Amekua akiiunga mkono kila ninacho kitaka CARA DELEVINGNE alimalizia.
Related posts
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…