Hatujui kama tuiite trend au ni muamko kutoka kwa watu maarufu, kwa sasa tumeweza ku-spot watu maaruufu wakiwa wamevalia mavazi kutoka kwa wabunifu wa hapahapa Nchini tena yakiwa yametoka straight from the runway.
Kwa hii trend/muamko sisi tunaufurahia kwa muda mrefu tumekuwa tukitamani wabunifu na watu maarufu kuungana na kufanya kazi pamoja hili kusaidiana katika kutangaza kazi kati yao.
Toka mwaka huu uanze tumeona watu maarufu na wabunifu wakishirikiana katika mavazi yao tumeona watu kama Wema Sepetu, Nandy Na Tanasha Donna wakiwa wamevalia mavazi kutoka kwa wabunifu kutoka Tanzania.
Wema Sepetu alivaa vazi kutoka kwa mbunifu Martin Kadinda, ambapo vazi hili linatoka katika “She Gentle Collection” ambayo ilikuwa debuted katika Swahili Fashion Week 2019 likiwa limevaliwa na mwanamitindo Anita.
Mwanamuziki na mwanamitindo Tanasha Donna yeye tulimuona akiwa amevalia straight from the runway outfits mara mbili, ambapo mara zote hizo alivaa mavazi kutoka kwa wabunifu kutoka Tanzania
Hapa akiwa amevalia off white jacket kutoka kwa mbunifu EK•AN•TIK kutoka katika collection yao ya mwaka 2019
Mara ya pili Tanasha alionekana kuvalia hizi animal prints two pieces kutoka kwa mbunifu Mahaumes, hii ameivaa katika music video ya wimbo wake mpya uutwao La Vie. Vazi hili lilikuwa debuted katika runways ya Swahili Fashion Week 2019 likiwa limevaliwa na mwanamitindo Lilian Loth hapa tumeona wameongeza matching top wakati kwenye runway ni skirt tu ndiyo ilikuwa imepitishwa.
Tumemuona pia mwanamuziki Nandy akiwa amevalia hii orange dress kutoka kwa mbunifu chipukizi Mahaumes, hili vazi alilivaa katika music video aliyoshirikishwa na mwanamuziki Ommy Dimpoz uitwao Tango. Gauni hili lilikuwa debuted katika runway ya Swahili Fashion Week 2019 likiwa limevaliwa na model Batuli Mohamed
Well Afromates tuambie unaoneje huu muamko wa wasanii na wabunifu kufanya kazi pamoja?
Related posts
5 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Find More Information here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/celebrity-living-the-straight-from-the-runway-life/ […]
… [Trackback]
[…] Information to that Topic: afroswagga.com/mitindo/celebrity-living-the-straight-from-the-runway-life/ […]
… [Trackback]
[…] Information to that Topic: afroswagga.com/mitindo/celebrity-living-the-straight-from-the-runway-life/ […]
… [Trackback]
[…] Read More here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/celebrity-living-the-straight-from-the-runway-life/ […]
… [Trackback]
[…] Info to that Topic: afroswagga.com/mitindo/celebrity-living-the-straight-from-the-runway-life/ […]