Week iliyopita kulikuwa na sikukuu ya Christmas ambapo baadhi ya watu maarufu walitoa picha zao ambazo zinaonyesha mionekano yao huku wakiwatakia wa-Tanzania sikukuu njema. Tunaweza kusema wengi wao walipendeza sana na kujitahidi katika mionekano yao, rangi ambayo ilitawala ilikuwa nyekundu.
Muigizaji Kajala Masanja alikuwa kwenye sequin dress kutoka kwa mbunifu Martin Kadinda, gauni hii ilikuwa na mpasuo mbele, Elizabeth Michael yeye alikuwa in gold & red dress kutoka kwa mbunifu @kenny_the_brand huku akiwa styled na brand yake ya @emclosettz lakini pia tuliwaona watoto wa producer P Funk Majani, Paula na Pataika wao walivalia ball dress za kijani na nyekundu.
Wengine ambapo walitupia picha zao lakini wao waliamua kuwa tofauti kidogo kwenye rangi ni Lulu Diva na Fahyma, ukiachana kuwa tofauti na rangi hawa wawili walipendeza sana na outfit zao.
Hatujajua nini kilitokea kwa mama Twins, Jacqueline Mengi but this outfit was and will always be a miss to us. She could peak kati ya viatu au kofia avae kimoja na kingine kipumzike.

Well Afromates tuambie outfit yako uliyoipenda ni ipi?
Related posts
HOT TOPICS
Happiness Magese Akionyesha Wanawake Warefu Namna Ya Kuwa Stylish: Kwa wanawake warefu huwa… https://t.co/VZ1jH2zJUg
FollowHappiness Magese Akionyesha Wanawake Warefu Namna Ya Kuwa Stylish: Kwa wanawake warefu huwa… https://t.co/689j7Yjcn0
FollowSubscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
Feza Kessy Atuelezea Kuhusu Fashion & Style Zake
Feza Tadei Kessy ni Muimbaji, Muigizaji lakini pia ni mtunzi wa nyimbo lakini pia Fezza ni former beauty queen ambapo mwaka 2005 alikuwa Miss Dar City Centre, Miss Ilala & Miss Tanzania Runner up. Lakini pia alishawahi kuwepo katika Reality Tv Show – Big Brother Africa. Kwa…