Imekuwa muda sasa tunasema fashion za Africa zinafika Duniani, tumeona wabunifu wakubwa wakitumia batiki, vitenge, shanga n.k katika collection zao, lakini pia tunaona vile watu maarufu kutoka Africa wanavyopewa collaboration na makampuni mbalimbali makubwa katika kazi zao, its our time to shine.
Ukiachana na wao kutengeneza bidhaa na kutumia malighafi yetu imeonekana wameanza sasa kuangalia na wabunifu kutoka Africa, leo tunakuletea mbunifu Claude Lavie Kameni ambae asili yake ni kutoka Cameroon lakini kwa sasa anaishi United States, Claude Lavie Kameni aliondoka Cameroon akiwa na miaka 8 na kwenda kuishi United States, wakati akihojiwa na asoebibella.com, Lavie alisema safari yake ya ubunifu ilianza alipokuwa mdogo ambapo akikuwa akichora, sketch na fashion design’s, wakati mwingine alikuwa akikata vitambaa na kuvigundisha, lakini pia alisomea kushona mavazi.
Mwaka huu umekuwa mwaka mzuri kwa Lavie ameweza kuwavalisha watu maarufu wakubwa wawili ambapo mara ya kwanza alimvalisha Janet Jackson dada wa marehemu Michael Jackson katika wimbo wake mpya wa Made For Now, hii ni come back song ya Janet as aliolewa na akapumzika kufanya muziki, watu wengi walikuwa wanataka kujua kuja kwake kupya atakuja na nini Janet amechagua kurudi akiwa na African touch’s and guess alivaa vazi kutoka kwa nani? you guess it right Lavie.
Lakini pia ameweza kumvalisha muigizaji Tracee Ellis Ross katika Tuzo za Ama’s, Tracee Ellis Ross alichagua kuvaa mavazi kutoka kwa black designer na kati ya wabunifu ambao alivaa mavazi yao mmoja wapo alikuwa Lavie, ambapo alimvalisha gauni la kitenge lenye fish tail na mikono ya tarumbeta, who would ever though a 8 years old kutoka Cameroon siku moja atakuja kumvalisha muigizaji mkubwa kama Tracee?
hii gauni pia ilishawahi kuvaliwa na muigizaji Tanika Ray kutoka kwa mbunifu huyuhuyu Lavie, lakini yeye aliivaa katika Red Carpet ya Premiere ya Black Panther
Lavie ni moja kati ya wabunifu wanao fanya vizuri kwa sasa na hupenda kutumia vitenge katika kubuni mavazi yake alipo ulizwa kuhusu kupenda kutmia African print hili ndio lilikuwa jibu lake
AsoEbiBella: Many designers shy away from prints, but you fully embrace it, bringing kente, dashiki and Ankara into mainstream American events like award shows and the likes. Tell us why prints speak to you so much.
Claude Kameni of Lavie by CK: The various African prints speak to me so much because I am a strong believer in the saying, “It doesn’t matter where you come from. But it matters most where you are going.” Wearing our prints to mainstream events and red carpets lets the world know that we are fully embracing who we truly are as people confidently and unapologetically.
Well kwa kusoma tulicho andika tulitaka tuwa motivate hasa wale wabunifu wanaochipukia au kama unafanya chochote katika kazi yako Lavie said it aliposema “it doesn’t matter where you came from but it matters most where you are going” jua unachotaka na jaribu kuweka malengo ya kufika mbali hakuna aliyejua kwamba iko siku huyu mbunifu atakuja kuvalisha watu maarufu kama Janet na Tracee lakini leo anaongelewa na milango yake ina funguka, humble begins matters, discipline katika kazi na malengo.
unaweza kumtafuta Instagram @laviebyck
Related posts
1 Comment
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Read More on that Topic: afroswagga.com/mitindo/claude-lavie-kameni-kutoka-cameroon-alivyoweza-kumvalisha-janet-jackson-na-tracee-ellis-ross/ […]