Navy Kenzo ambalo ni group la wasanii wawili Aika na mpenzi wake Nahreel wametoa wimbo mpya uitwao Fella, Well tumeona video yake na we are impressed the video is very fashionable ni kama unaangalia run way, japo wimbo ni mzuri lakini pia mionekano yake humu ndani imefanya video kuvutia zaidi, hivi ni baadhi ya tulivyopenda kutoka katika video hii,
Wametumia stylist wawili ambao ni Macrida na Noel Ndale – hii inaonyesha kabisa walijipanga kupata kitu kizuri japo stylist mmoja angetosha lakini walitaka ideas mbalimbali, unaweza kuona video ina washiriki wengi kama wangetumia stylist mmoja angeweza kuharibu sehemu lakini kwa sababu walikuwa wawili wameshirikiana kutoa kitu bora. Kudos kwa hili.
Stylist wametumia wabunifu kutoka Tanzania – katika hii video kuna mavazi ya designers watatu kutoka Tanzania ambao ni Kiki Designs, Samuel Zebedayo na The Agnes kwa kipindi kirefu tulikuwa tunalilalamikia hili swala lakini kidogo kidogo tunaona linaanza kufanyiwa kazi hii video ina stahili kuwa fashionable video Navy Kenzo wame invest sana ni haki kupata kilicho bora.
Wametumia mavazi ya asili na kisasa – kwenye video kuna ambao wamevaa vitenge lakini pia kuna ambao wamevaa jeans na vintage shirts, tumependa hii combination, kama ukiangalia kinacho trend Duniani kwa sasa ni kurudi kwa 90’s na hii video inatupa vibe hiyo.
Matumizi ya Models wa ki-Tanzania – hiki ni kingine ambacho Navy Kenzo wametufuraisha kutumia wanamitindo wa kwetu & inabidi tusema hawa wanamitindo wamejitahidi sana humu tumeona efforts, kuanzia ku-pose, kuonyesha mavazi lakini pia ku-have fun.
Color Coordination – upangaji wa rangi wa mavazi umetulia, rangi zimeendana na maudhui wa wimbo. Wimbo ni kama reggae fulani hivi na kama ambavyo tunajua reggae imetoka Jamaica na wao huwa wanatumia rangi katika video zao, tumependa kwamba hawakwenda too Jamaican katika mavazi lakini wakatupa ile vibe ya Caribbean
African Accessories – katika video kuna aina mbalimbali za accessories kuna turban za kitenge, shanga za kimasai etc. lakini pia walitumia na accessories za kisasa
Tunaipa hii video 9.5 kwa sababu tu wanasema “nothing is perfect” lakini kwetu sisi tunasubiri msanii ambae anaweza kufanya zaidi ya hii maana Navy Kenzo ni kama wamekomoa hivi. unaweza kuingalia hapo chini na kutupa maoni yako
Related posts
5 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Find More Info here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/collaboration-ya-noel-ndale-na-macrida-joseph-katika-video-ya-fella-ya-navy-kenzo/ […]
… [Trackback]
[…] Find More on on that Topic: afroswagga.com/mitindo/collaboration-ya-noel-ndale-na-macrida-joseph-katika-video-ya-fella-ya-navy-kenzo/ […]
… [Trackback]
[…] Read More on that Topic: afroswagga.com/mitindo/collaboration-ya-noel-ndale-na-macrida-joseph-katika-video-ya-fella-ya-navy-kenzo/ […]
… [Trackback]
[…] Read More Information here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/collaboration-ya-noel-ndale-na-macrida-joseph-katika-video-ya-fella-ya-navy-kenzo/ […]
… [Trackback]
[…] Read More Information here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/collaboration-ya-noel-ndale-na-macrida-joseph-katika-video-ya-fella-ya-navy-kenzo/ […]