SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Color Hacks For A Killer Outfit – Part 1
Mitindo

Color Hacks For A Killer Outfit – Part 1 

Moja kati ya vitu ambavyo vinapandisha na kushusha outfit yako ni mpangilio wa rangi, zinaweza kuharibu kabisa muonekano wa vazi lako kama zitapangiliwa vibaya na zinaweza kufanya vazi lako litoke kutoka 0-100 real quick. Wengi huwa tunazikimbia kutokana na kuto kujua namna ya kuzipangilia ili kupata muonekano mzuri tunachagua kuwa kwenye comfort zone ya rangi zilezile na kuto kutoka zaidi ya hapo well leo tunakuletea namna 3 kati ya 6 tulizoziandaa ya jinsi ya kutumia rangi katika muonekano wako na ukaonekana vizuri.

Lets Hack Them

 • Take Baby Steps / Power Of Contrast 

Kama ambavyo tulisema mwanzo rangi zinaweza kupandisha na kushusha muonekano wako kwa hiyo instead ya kuharakisha kuanza kutumia rangi nyingi kwenye outfit moja unaweza kuanza na step ndogo ndogo kama kuanza kuvaa a statement bright color na dark colors, eg unaweza kuvaa vazi la rangi nyeusi tupu ukaongezea na viatu au blazer yenye rangi kidogo.

Kama hapa ambapo tunamuona style blogger style pantry akiwa amevalia rangi zilizo tulia akiwa amemalizia na viatu ambavyo vina rangi kali, viatu vimekuwa kama statement na attention imehamia kwenye miguu wakati juu akiwa simple tu mavazi yake.

Hapa aliamua hii top yake ya neon yellow ndio iwe statement katika vazi lake huku akimalizia muonekano wake na neutral colors

 • Monochrome Colors 

Ukitoka kwenye baby step unachoweza kufanya baada ya hapo ni kuvaa monochrome colors yaani kuvaa vazi la rangi moja juu mpaka chini, hii inasaidia kutokuonekana una mambo mengi au rangi nyingi katika outfit moja, unaweza kuchagua kuvaa rangi nyeupe juu mpaka chini, nyekundu etc rangi yoyote inawezana kuvaliwa na bado ukaonekana umetumia rangi lakini haupo too much

Unaweza kutumia rangi ambazo zimetulia kidogo sio ziwe neutral kabisa  unaweza kutumia light to dark colors kama alivyofanya Chinyere Chi-Chi Adogu na hii purple lavender color

Au ukatumia bright colors kama yellow, green au yoyote kama ambavyo simply palesa amefanya na outfit yake, ametumia shade moja ya rangi ya njano kuanzia viatu mavazi na funny pack wakati kwenye accessories ameamua kutumia dark yellow.

 • Pick A Common Color 

Unapovaa colorful outfit iwe floral, stripes au outfit ya zangi tofauti unahitaji kuchagua rangi moja iliyopo katika outfit hio ambayo itafanya outfit ionekane putted together, one common color ambayo itaonekana mara nyingi kufanya outfit yako iongee rangi hio. Unaweza kubeba mkoba wa rangi hio, kuvaa hereni, miwani,saa, au hata blazer ya rangi hio ilimradi hio rangi ionekane ndio rangi kuu ya vazi lako.

Simply Palesa hapa alichagua hii rangi ya njano iliyopo katika two pieces zake ndio iwe rangi kuu kwa kuongezea viatu, waist bag na hereni zenye rangi ya njano.

Kuwa na sisi tena wiki ijayo wakati tukikuletea sehemu ya pili na ya mwisho ya tips hizi, kama una tatizo katika fashion, style na beauty na ungependa tuliongelee tuandikie katika box la comment au katika account zetu katika mitandao ya kijamii

 

Related posts

5 Comments

 1. 7up gummies

  … [Trackback]

  […] Find More Information here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/color-hacks-for-a-killer-outfit-part-1/ […]

 2. roof skylight

  … [Trackback]

  […] Find More here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/color-hacks-for-a-killer-outfit-part-1/ […]

 3. 빗썸

  … [Trackback]

  […] Info to that Topic: afroswagga.com/mitindo/color-hacks-for-a-killer-outfit-part-1/ […]

 4. 티비위키

  … [Trackback]

  […] Info to that Topic: afroswagga.com/mitindo/color-hacks-for-a-killer-outfit-part-1/ […]

 5. Golden Teacher Mushrooms

  … [Trackback]

  […] There you will find 54120 additional Information on that Topic: afroswagga.com/mitindo/color-hacks-for-a-killer-outfit-part-1/ […]

Comments are closed.