Wakati mwingine kuongeza rangi katika mtoko wako kuna sababisha siku yako iwe njema kabisa, a little touch of color can change your mood. Wakati mwingine unaweza kuamka na siku mbaya kabisa inabidi ujaribu kutafuta kitu gani kinaweza kufanya siku yako ibadilike, na kitu rahisi ni ku-add color kwenye mtoko wako lakini unapo kuwa na siku mbaya na ukavaa rangi za kufifia (kama nyeusi,damu ya mzee etc)bado utaendelea kujihisi vibaya, katika pita pita zetu tumekutana na hawa Fashionistas ambao tumependa jinsi walivyo changanya rangi katika mitoko yao

Fashion Blogger  @swaggaismything yeye ametuonyesha uwezo wake wa kuchanganya rangi kwa kuvaa suit yenye rangi ya baby yellow, huku akiwa amevalia na viatu vya pink akimatch na pochi ya pink amemalizia muonekano wake na accessories (pete, miwani na bracelet) huku akiwa ame pop orange lipstick, unaweza kuona namna amechanganya rangi tatu zinawowaka bila kuwa too much.

Fashion Blogger mwingine anaependa rangi @SimplyCyn, yeye amevaa mustard sweater, suruali nyekundu huku akiwa amebeba pochi ya orange, amemalizia muonekano wake na lipstick nyekundu na huge ring earrings unaweza kuona uwezo wake wa kuchanganya rangi sio kila mtu anaweza kuvaa rangi zote hizi na kuonekana this cute. unaweza kujaribu pia.

Fashion Blogger kutoka angola @angodiva  yeye aliamua kutumia viatu na suruali kubrighten muonekano wake, ambapo alivaa suruali nyekundu, open heels nyekundu pia huku akiwa amemalizia muonekano wake na black & white polka dot blouse na black clutch.

Green & orange on @SimplyCyn,

Hivi ndivyo namna unaweza kuongeza rangi kwenye mionekano yako kama wewe ni mpenzi wa rangi.

 

Comments

comments