Mwaka jana mwezi wa tisa Queen Bee au kwa jina lake la kuzaliwa Beyonce alitu-bless na tour ya Otr 11 ambapo ukiachana na show zake kusifiwa na ku-trend Beyonce alianzisha trend kadhaa za mavazi ikiwepo kuzirudisha kwenye trend hizi Cartwheel hat, alizivaa mara kwa mara katika tour yake hiyo na tulijua zitakuwa trend which kutoka September mpaka sasa bado tunaendelea kuziona.
Kwenye tour yake hii Beyonce alivaa hii leopard print bodysuit ambayo ili include large hat pamoja na boots, akiwa katika tour yake mjini London, outfit hii imeonekana kuwavutia wasanii wengi na kuwa wanatumia katika video zao, kitu ambacho kwetu tumeona tukiweke hapa tukiongee
Mwezi March mwaka huu tulimuona mwanamuziki Nina Roz kutoka Uganda akiwa ameshoot video yake iitwayo Munda Dala akiwa kwenye outfit kama ya Beyonce kasoro tu yeye hakuwa na boots chini, we said to our self Afro take a chill pill its okay to be inspired tukaamua kunyamaza na kauicha ipite
Mwezi mmoja ukapita First Lady Wa WCB, Queen Darleen akatoa wimbo wake uitwao Muhogo, humo ndio kuna balaa amecopy outfit nyingi kutoka kwa wasanii wakubwa mbalimbali akiwepo Beyonce , tulikuwa tagged na watu wengi wakaomba tuongelee, tukasema hamna ha kuongelea maana hatuna kizuri cha kuongelea kuhusu video hio. Na yeye pia alivaa hili vazi ambalo linaendana excactly na la Beyonce kasoro tu ya Queen Darleen ilikuwa ni cheap version
Na juzi tu hapa mwezi huu mwanamuziki Lulu Diva nae ameonekana kwenye outfit inayoendana na hii hii katika video ya wimbo wake wa mapopo, yeye alimua kucheza nayo kidogo kwa kuvaa one shoulder jumpsuit na kofia
Well hii imetufanya tuwaze ni kweli uwezo wetu wa kufikiri kuhusu fashion & style ndio unaishia hapa? kwanini tunaona copy cat ni kitu kizuri? Kwanini tunasubiri wengine wafanye na sisi tufuate? Hatuwezi ku-create cha kwetu au kuwa inspired kufanya bora zaidi ya wenzetu bali sisi tunakomaa na mediocrity? hizi ni video tatu na zime kuwa styled na stylist tofauti tofauti Je? Stylist wetu mnafanya nini? is this the best you can do? Hii industry itakuwa kwa ku-copy watu wengine?
Afromates lets sip this coffee and discuss je hii ni sawa?
Related posts
HOT TOPICS
Happiness Magese Akionyesha Wanawake Warefu Namna Ya Kuwa Stylish: Kwa wanawake warefu huwa… https://t.co/VZ1jH2zJUg
FollowHappiness Magese Akionyesha Wanawake Warefu Namna Ya Kuwa Stylish: Kwa wanawake warefu huwa… https://t.co/689j7Yjcn0
FollowSubscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
Feza Kessy Atuelezea Kuhusu Fashion & Style Zake
Feza Tadei Kessy ni Muimbaji, Muigizaji lakini pia ni mtunzi wa nyimbo lakini pia Fezza ni former beauty queen ambapo mwaka 2005 alikuwa Miss Dar City Centre, Miss Ilala & Miss Tanzania Runner up. Lakini pia alishawahi kuwepo katika Reality Tv Show – Big Brother Africa. Kwa…