SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Dalili 3 Unajiachia Kimuonekano (Letting Yourself Go)
Mitindo

Dalili 3 Unajiachia Kimuonekano (Letting Yourself Go) 

Tumesha sikia au kulitumia hili neno mara nyingi, unaweza kuwa umekutana na mtu ambae ulikuwa unamjua zamani akakwambia umejiachia au wewe ukajiuliza kwanini huyu amejiachia hivi? Lakini ukajiuliza hili neno kujiachia ni nini au kwanini huyu mtu amekwambia hivyo au ameona nini mpaka akasema haya maneno?

Kwanza tujue kujiachia ni nini?

Kujiachia kama ambavyo lipo yaani upoupo tu inawezekana umejiachia kimavazi au kimwili kuna msemo huwa unasema “Upo upo tu Duniani haupo na Akhera wanakutafuta” hii ni maana nzuri ya kujiachia lol. Well ni nini utaona kujua sasa nimejiachia?

  • Hujijali

Hukumbuki mara ya mwisho lini umekaa ukapumzika vyema, upo kila mahali ukiamka wewe ni mwenda wa kuzurura leo upo huku kesho upo kule huna siku ambayo unasema upumzike na kujali mwili wako, huangalii unachokula unajilia tu chochote au una skip kula basi jua umejiachia.

  • Unakasirika haraka

Je ni moja kati ya wale watu kitu kidogo tu kinakuudhi? umeacha stress za maisha zichukue furaha yako na kuondoa nuru katika maisha yako? unatembea umekunja sura bila sababu maalum? Hutaki kuonana na watu unaona kero wakati mwingine hata unajificha usikutane watu? jua umejiachia

  • Umeacha kujali kuhusu muonekano wako

Hukumbuki mara ya mwisho umekaa ukaangalia mavazi gani ya kuvaa, hukumbuki mara ya mwisho umejali ngozi yako au muonekano wako, basi jua umejiachia na huna habari na mwili au muonekano wako.

Related posts