SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Date Outfit Ideas From Juma Jux And Karen Bujulu
Mitindo

Date Outfit Ideas From Juma Jux And Karen Bujulu 

The weekend is here inawezekana una plans za kutoka na mwenza wako, lakini hujui uvae nini unapoenda, well kuna date’s za aina tofauti tofauti kuna za casual, business na zile romantic zote hizi zina mitoko yake kutokana na sehemu mnayoenda.

Leo tunawaangalia couple mpya kabisa ambayo imeenda instagram official miezi michache iliyopita na sio wengine bali ni mwanamuziki na mfanyabiashara Juma Jux pamoja na mpenzi wake Karen Bujulu as we all now Juma anapenda fashion na kwa kufutatilia page ya Karen yeye pia hayupo nyuma kwenye maswala ya mitindo.

Tumeona mitoko yao wakiwa wameenda sehemu mbalimbali tukaona tuwaletee hapa incase mngependa kuvaa kama wao au kujua mavazi waliyovaa mnaweza kuvaa wapi.

Casual date

  • hii ni date ambayo mara nyingi ni mchana au jioni ambapo mnaenda kutembea sehemu za kawaida kama kuangalia movies, kucheza games, kuangali games (basketball, football) au hata evening walk tu. Unaweza kuvaa kama Jux na Karen, denim look ambapo sio sexy wala sio casual sana.

Business Date

  • hii ni ile date ya ki-biashara zaidi inaweza kuwa mnatoka na wafanyakazi wenzenu au mna kutana na wafanyabiashara wenzenu hapa hutakiwi kuwa too official au too sexy unatakiwa u-balance kati ya official na sexy kama ambavyo una balance shobo (jokes) ukiangalia hapa namna Karen ame style suit yake amevaa white suit lakini hajavaa shirt ndani kaonyesha cleavage lakini sio ile too much na ameongezea na statement necklace na kwa Jux alivaa suit akatupia na trench coat.

Romantic date

  • hapa sasa mko wawili tu mkienda kunogesha pendo lenu inaweza kuwa mnaenda kula dinner, mnaenda kusikiliza live music sehemu classic etc basi ni vyema ukaenda extra na look yako be sexy show some skin, makeup nzuri na kwa mwanaume unaweza kuvaa suit / tuxedo yako huitaji kuwa too formal look hii ya Jux ni mfano tosha

Well ni matumaini yetu tumekusaidia, tuambie ulivaaje kwenye date yako kupitia account zetu za mindao ya kijamii (instagram, twitter na facebook)

Related posts