Mwaka jana mwezi wa tatu brand ya Louis Vuitton ilimtangaza Virgil Abloh kuwa creative director mpya wa department yao ya menswear, hii ilitokana na Kim Jones ambae alikuwa creative director wa department hio kuamua kuondoka, Mwaka jana huo huo June, Virgil Abloh alishow case collection ya kwanza ya Louis Vuitton akiwa kama creative director katika Paris Fashion Week.

Moja kati ya vitu tulivyo viona katika collection hio ni hizi travelling bags ambazo zimepewa jina la M53271  keepall baundouliere 50, zipo za rangi tofauti tofauti lakini zilizoonekana kuvutia wengi ni hizi za silver zenye kung’aza.

Bags hizi ukiingia kwenye website ya Louisvuitton.com zinauzwa Eur 2,520 sawa na fedha za kitanzania sh Million 6,470,757.09/-  enhe unaweza kuwa mtaji ukafungua kiduka chako cha nguo cha bidhaa ndogo ndogo,

Tumemuona mwanamuzi kutoka Nigeria, Davido Adeleke akiwa amebeba hii bag, huku akiwa ameweka caption ya “A week early for Fashion week”  huku location yake ikiwa inasoma Paris France.

Alibeba Bag hii akiwa amevalia embellished white shirt, suruali nyeusi akamalizia na hii statement bag, black shoes na accessory ndogo ndogo.

Tunapenda siku hizi Davido anajaribu sana katika mavazi yake, but wait kuna kitu tukitegemee kutoka kwake kwenye Paris Fashion Week mwaka huu? May be yes or may be not we will keep our eyes open and be sure to notify you.