Inawezekana uliifuatilia hii harusi kwakina kabisa na ukapenda baadhi ya mavazi (gauni) aliyoyavaa Nandy na hujui yalitoka wapi au unaweza kuyapata wapi,well hizi ndizo details tulizozipata kuhusu magauni aliyoyavaa Nandy.
Kitchen Party Dress by Elisha Red Label


Nandy alivalishwa na mbunifu kutoka Tanzania Elisha Red Label, alivaa gauni nyekundu aliyomatch na head piece.
Send Off Dress by Valdrin Sahiti


Kwenye sendoff yake Nandy alivaa blue feather dress kutoka kwa mbunifu Valdrin Sahiti anaetokea Nchini, Kosovo tunaweza kusema gauni imepanda ndege kwa masaa kadhaa mpaka kufika Tanzania, mbunifu huyu ndiye aliyemvalisha Elizabeth Michael katika harusi yake pia.
Wedding Dress By Nandy Bridal


Wedding dress ilikuwa off white ball dress yenye ming’ao, the best feature ya hii gauni ni style ya mkono wake ambapo ilikuwa kama majani, it was a beatiful dress hasa ukiiona kwenye video. Gauni imetoka kwenye duka lake la Nandy Bridal ambapo inatufanya tuamini imetoka Turkey maana huko ndipo anapochukulia magauni yake lakini pia tuliona alienda kufanya shopping huko.
Reception Dress by Elisha Red Label


Baada ya ndoa kanisani Nandy na mumewe walienda ukumbuni mlimani city ambapo ilifanyika sherehe yao, Nandy alibadilisha gauni akavaa dress ambayo iliweka gumzo kidogo mtandaoni kutokana na kuonyesha baadhi ya viungo, na gauni hii ilitoka kwa mbunifu kutoka Tanzania Elisha Red Label, jiandae na interview yake itakayokuwa hewani muda sio mrefu.
Related posts
3 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Read More here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/details-on-nandys-kitchen-party-sendoff-wedding-dresses/ […]
… [Trackback]
[…] Read More on that Topic: afroswagga.com/mitindo/details-on-nandys-kitchen-party-sendoff-wedding-dresses/ […]
… [Trackback]
[…] Find More here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/details-on-nandys-kitchen-party-sendoff-wedding-dresses/ […]