SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Dhambi 3 Za Fashion Inazofanywa Na Wanaume
Mitindo

Dhambi 3 Za Fashion Inazofanywa Na Wanaume 

Kwenye fashion mistakes ni ngumu sana kukosekana kwa sababu mbali mbali ambazo zinaweza kufanyika kwa kujua au kwa kutokujua. Wanaume wengi huwa wanafanya mistakes katika mionekano yao ya kila siku na hivyo upelekea kupunguza mvuto wa muonekano wote. Kuna makosa mengi sana ambayo yanapelekea kuharibu muonekano wa mwanaume na kuna muda inaweza kupelekea kukosa madeals makubwa kutokana tu na style yako.

1. Too much Matchy matchy

Ni moja ya mistake katika style ambayo kila mtu anajua kuwa ni mistake kwa sababu unamkuta mtu kavaa chini mpaka juu blue au kavaa rangi ambazo akionekana basi anakuwa kama kituko kutokana na sababu mbalimbali za kudhani ili nipendeze ni lazima nivae matchy match

Kuvaa matchy matchy unaonekana wa kawaida sana na hauvutiii kwa sababu umeshindwa kuchagua great combination ya rangi ambazo zitafanya style yako iwe ya kipekee na inayovutia mda wote. .

2. Oversize shoes

Hii ni too common sasa maana wanaume hawataki kubadilika kwa sababu kitendo cha kuvaaa oversized shoes inakufanya uonekane style yako isiwe na msisimko hata kidogo, unaweza ukawa umevaa vizuri sana lakini mguuni viatu vinaonekana vikubwa sana na kufanya watu waweke attention yote kwenye mistake ambayo umefanya. Vaa viatu ambavyo vinakufit well hili ufanye style yako ionekane well organized.

Note: shida sio mistakes lakini hizi ni mistakes ambazo unatakiwa uziepuke kwa sababu ya kulinda your personal style isiwe na makosa mengi na kukufanya uwe well organized. Unaweza kutuambia ni common mistake gani ambayo ulikuwa unafanya kabla ya kusoma hii article .unaambiwa tunanunua mavazi ila hatuwezi kununua style kwa sababu style inakuwa created na wewe mwenyewe.

3. Wearing competing brands together

Unaweza ukajiuliza kivipi inaweza kuharibu style yako basi ni jambo dogo sana. Nadhani,Umeshawai kuwaona wanaume wamevaa full tracksuit ya adidas then chini wakavaa Nike hapo anakuwa kafanya mistake kwa kujua au kwa kutokujua kwa sababu nike pia wanatracksuit na wapo na competing na adidas. Unaweza usione kama ni mistake ila ingekuwa vizuri ungevaa full outfit ya brand moja au brands ambazo sio competing na ungeonekana upo well organized.

Imeandikwa na @gotchathegreatest

Related posts