SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Diamond Platnumz Kuvaa Kikuku Je Ni Sawa?
Mitindo

Diamond Platnumz Kuvaa Kikuku Je Ni Sawa? 

Kama kuna kitu ambacho huwa kina make headlines katika jamii ni kwa mwanaume kuvaa kitu ambacho kinaaminika kina paswa kuvaliwa na mwanamke tu, hii hufanya watu kumdharau na kushusha heshima yake kama mwanaume. Weekend iliyopita mwanamuziki Diamond Platnumz ame make headlines baada ya kuvaa kikuku ( shanga ya mguuni), wengi walionekana kutokuvutiwa na hiki kitu.

But oh well oh well isn’t this 21 century though? people do what they want hakuna boundaries au limit cha huyu kisivaliwe na huyu unless ni wewe mwenyewe ujiwekee kwamba siwezi kuvaa hiki, to think of it wanaume wanavaa hereni, vipini vya pua na wengine sasa hivi wanavaa skin jeans?

Diamond Platnumz si wa kwanza kuvaa kikuku tulisha muona mume wa muigizaji Gabrielle Union, Dwayne Wade akiwa amevaa kikuku tena yeye aliibuka nacho kwenye red carpet na suit juu

Lakini pia mwanamuziki Chris Brown alitupia picha yake siku kadhaa nyuma akiwa ameonyesha mguu wake akiwa amevaa kikuku cha vito

lakini pia kuna baadhi ya makabila Africa na Nje ya Africa huwa wanavaa vikuku mfano mzuri wa makabila haya ni wamasai wao mwanaume kuvaa kikuku sio big deal.

Hatupingani na wanaosema Diamond kuvaa kikuku ni kitu kibaya na wala hatusemi ni kitu kizuri tunacho sema kila mtu ana mipaka yake na jinsi anavyo ona vitu, kama yeye kaona ni sawa basi ni sawa kwake as long as he is comfortable with it. The only thing we can say is fashion inakua na mipaka inazidi kuvunjwa ni wewe na akili yako kuona mpaka upi usivuke but if its okay kuvuta you do you in the name of FASHION.

Tuambie wewe kuona Diamond amevaa hivi ni sawa au lah kama mtu anae angaliwa sana na vijana wa kiume? Kwa wanaume ambao mnafuataga au kuiga style za Diamond Platnumz utaiga hili?

 

Related posts