SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Doreen Mashika Latest Collection Is Fabulous In Every Way
Mitindo

Doreen Mashika Latest Collection Is Fabulous In Every Way 

Doreen Mashika ni moja kati ya wabunifu wanaofanya kazi nzuri kabisa hapa Nchini kwetu, hivi karibuni tumeona collection yake mpya ambayo amei-showcashe nchini Africa Kusini. Collection hii ilituvutia kutokana na umaridadi wake na mpangilio wa mavazi haya, tume mtafuta Doreen na kuweza kujua mawili matatu kutoka kwake kuhusu collection hii,
Afroswagga:  Always umekuwa unique katika uchaguzi wa fabrics. This time what inspired you katika kuchagua fabric, na unanunuaga wapi fabric zako as wabunifu wengi huwa wanalalamika kuwa ukosefu wa material ndio unasababisha wao kutumia fabric zinazojirudia?
Doreen: KAMA INAVYO FAHAMIKA KUWA ZANZIBAR NI SEHEMU MOJA YA KIPEKEE NA HIO NI PAMOJA NA KHANGA ZAO AMBAZO ZINAPATIKANA SEHEMU NYINGI NDANI YA MJI MKONGWE. SWALA LA KUWA NA UKOSEFU WA VITAMBAA NI LA UKWELI ILA TANGU AWALI NILIKUWA NIKIPENDA KHANGA HIVYO NAJIKUTA NIKINUNUA NYINGI MNO NA KUZIWEKA HATA ZAIDI YA MIAKA MITATU KISHA NIKIWA KARIBU NA SHUGHULI YA MITINDO NINAJIKUTA NINA ANZA KUCHAMBUA KHANGA ZA ZAMANI AMBAZO HAZIPATIKANI TENA SOKONI. HIVYO BASI KILA SAA HUONEKANA KUWA BRAND YA DOREEN MASHIKA NI YA KIPEKEE AFRICA MASHARIKI KWANI MTU AKIZITAFUTA HAZIONI TENA. ILA NJIA HII PIA NI GHALI KATIKA BIASHARA LAZIMA NIWE MKWELI.
Afroswagga:   Jina la hii collection mpya ni nini na linamaanisha nini?
Doreen: COLLECTION HII NI NO NAME MAANA SIKUWA NA MUDA HATA WA KUITUNGIA JINA ILA KITU KIMOJA NILIJUA KUWA LAZIMA ZIWE ZANZIBAR KHANGA.
Afroswagga: Ulimfikiria mwanamke wa aina gani wakati una andaa hii collection?
Doreen: MADHUMUNI YANGU KAMA ILIVYO KAWAIDA YETU MWANAMKE ANAKUA KATI Y MIAKA 27-70 NA BAADA YA HII SHUGHULI YA MITINDO CAPETOWN, AFRICA KUSINI TUNAJIKUTA KUWA HATA WASICHANA WENYE UMRI MDOGO KAMA 13 WAZAZI WAO WANAULIZIA NGUO ZETU NA KUTAKA KUWANUNULIA KITU AMBACHO NI KIPYA KWETU ILA KINATOA ISHARA NZURI KIBIASHARA YA KWAMBA  NGUO ZETU ZIMEKUBALIKA KIPINDI HIKI ZIMEKUBALIKA ZAIDI.
Afroswagga:  How long ilikuchukua kukamilisha collection hii and most of the inspiration uliipata wapi?
Doreen: NIA ILIKUWA KUTENGENENZA NGUO NYINGI ZAIDI YA ULIZO ONA ILA MUDA ULIKUWA MFUPI NA KAMA ILIVYO DESTURI NCHINI UKATIKAJI WA UMEME ULILETA CHANGAMOTO WAKATI WA UFULISHAJI  HIVYO, UBUNIFU, KUTOA PATTERN NA KUFULISHA  PISI 10 ILICHUKUA TAKRIBAN SIKU 14. UBUNIFU WANGU ULITOKA ZAIDI KATIKA HISTORIA YA KIZANZIBARI IKIWA SI TU KHANGA LAKINI HATA UREMBO WA POCHI ZETU ZILIKUWA NA NEMBO YA ZANZIBAR DOORS.
Afroswagga: Ni vipi ulikabiliana na vikwazo hivyo?
Doreen: TULIJIKUTA TUKIFANYA KAZI OVERTIME
Afroswagga: Huwa unadeal vipi na pressure katika uonyweshaji wa mavazi katika majukwaa makubwa nje ya nchi?
Doreen: HUWA NAENDAGA NA ATTITUDE YA  MAREHEM  DR MENGI (RIP)  AMBAYO NI …. I WILL … I CAN ….I MUST USIPO JIAMBIA NA KURUDIA HAYO MANENO KIMOYO MOYO UTAENDA NA WOGA NA UNAWEZA USIFANIKISHE.
Afroswagga: Mara yako ya kwanza katika international runway ilikuwaje? How was the experience? The goods and bads
Doreen: MAAJABU NI KWAMBA ILIKUWA NI NZURI NA PALIKUWA NA WANAMITINDO TOKEA AFRICA MASHARIKI NA MAGHARIBI NA KARIBU WOTE WALIKUWA NA UZOEFU SI CHINI YA MIAKA 10. MAAJABU NI KWAMBA WAANDISHI WA HABARI WALINIFWATILIA MNO KWANI NILIKUWA NI MCHANGA KATIKA MAMBO YA MITINDO HIVYO IKAWA NI FAIDA SANA KWANGU NA VILE VILE KWAKUWA WABUNIFU WAKISHA JIAMINI SANA HUKU AFRICA UNAKUTA WAKIJA WAMECHELEWA AU UNAKUTA MTU HAJI KABISA BASI NA MIMI KWAKUWA NI MTU AMBAYE NINA SIFA YA SWISS TIMING YAANI SICHELEWI HATA PUNJE KIKAZI NIKAJIKUTA WAANDISHI WA HABARI WENGI WALINIPIGA INTERVIEW BILA HATA YA KUTEGEMEA KWAKUWA NILIKUWA NIMEFANYA VIZURI NA NIKIWA MCHANGA KATIKA MAMBO YA MITINDO YA MAVAZI.  BY THE TIME PRESS INATOKA IKAWA KILA PAHALA DOREEN MASHIKA ZANZIBAR INA NGARA KUANZIA KWENYE MAGAZETI NA KWENYE RUNINGA.
Afroswagga:  Unaonaje maendeleo ya wabunifu wengine ulipokuwa huko?
Doreen: NI MAZURI NA UNAKUTA WENGINE WANATOKA NCHI ZA AFRICA AMBAZO WANA VIWANDA VIKUBWA NA VIDOGO HIVYO KILA MBUNIFU ANA BUNI NA KUFULISHA KUTOKANA NA UWEZO WAKE IKIWA NI FAIDA MOJA WAPO KWANI UNAKUWA NA UWEZO WA KUKOMAA KATIKA KAZI YAKO KAMA MBUNIFU TU. ILA TANZANIA NI TATIZO MAANA UNAKUWA MBUNIFU, MWENDESHA KIWANDA NA MAFUNDI KITU AMBACHO SIO TU GHARAMA ILA SIO KILA MTU ANA UWEZO KIFEDHA, KIMUDA NA UFANISI WA KUENDESHA NA KUMANAGE MAFUNDI NA KIWANDA KIDOGO. HII PIA INAKUWA CHANGAMOTO
Afroswagga: Can Tanzanian designers keep up with the international scene?
Doreen: WABUNIFU WAPO ILA CHANGAMOTO NI NYINGI HIVYO WENGI HUKATA TAMAA. NDIO MAANA TUPO WACHACHE.
Afroswagga:   Tutegemee Doreen Mashika Store Tanganyika pia?
Doreen: KWA SASA SINA UHAKIKA LINI ILA SI KITU CHA KUFUNGIA MACHO KWANI YAWEZEKANA NIKAJA HUKO BARA. ILA KWA SASA TUPO UNGUJA MAGHARIBI, NDANI YA  MJI MKONGE, MTAA WA SHANGANI, ZANZIBAR
Afroswagga: Chochote ambacho ungependa kukiongelea au kukiongezea
Doreen: XXXXX ASANTE KWA SASA NA SHUKRAN.

Related posts

2 Comments

  1. shroomies edibles

    … [Trackback]

    […] Find More on that Topic: afroswagga.com/mitindo/doreen-mashika-latest-collection-is-fabulous-in-every-way/ […]

  2. buy ayahuasca tea online jumia,

    … [Trackback]

    […] Here you can find 79734 additional Information on that Topic: afroswagga.com/mitindo/doreen-mashika-latest-collection-is-fabulous-in-every-way/ […]

Comments are closed.