Unapoanza kubadilisha style au kuboresha style ni muhimu kuanza na capsule wardrobe. Unaweza kuitengeneza kwa nguo mpya, za zamani au mix ya nguo mpya na za zamani. Capsule wadrobe ni set ya nguo chache za msingi unazoweza kuvaa zenyewe kama zenyewe au na nguo nyingine. Unaweza kumatch na kumix nguo chache katika capsule wadrobe kutengeneza looks nyingi.
Kuwa na capsule wardrobe kunakuhakikishia kuwa na nguo za muhimu kwa ajili ya kitu fulani au tukio fulani mfano: capsule ya nguo za kazi, capsule ya nguo za mitoko, capsule kiujumla. Ukiwa na capsule huwezi kukosa cha kuvaa au nguo ya kuvaa na nguo nyingine. Kukupa picha naassume leo natengeneza capsule kwa ajili ya dada anayefanya kazi katika shirika la kifedha, dada anaitwa Lisa, Capsule ina sifa hizi na mifano itakuwa kwa ajili ya capsule ya Lisa;
Ina nguo za rangi fulani tu
Mara nyingi capsule wardrobe huwa na rangi zinazoendana na rangi nyingine zote kama rangi nyeupe, nyeusi, kijivu, brown, dark blue, off white au cream na nudes aina zote. Rangi zake huwa zimetulia na nguo inakuwa na rangi moja. Lisa anapenda zaidi rangi nyekundu na blue. Rangi nilizotaja kwa ajili ya capsule huendana na rangi zote kwaio zitaendana nae
Ina nguo bora zinazoweza kuvaliwa na nguo nyingine nyingi
Nguo nyingi katika capsule wadrobe ni zile ambazo unaweza kupair na nguo nyingine nyingi. Ni nguo rahisi kuvaa na kustyle. Nguo hizi huwa hazina miundo wala rangi za kipekee bali kawaida tu. Lisa kama mfanyakazi katika sekta maalumu anaweza kuwa na kabati yenye hivi:
Suruali za kitambaa tatu; nyeupe, nyeusi, brown.
Jeans mbili, dark bule na blue iliyopauka (siku za ijumaa, mitoko ya kiofisi, sports day e.t.c)
Tshirt tatu; nyeupe, nyeusi, brown plain zisizo na michoro.
Shati mbili, nyeupe na nyeusi.
Blauzi mbili za chifon, dark blue na brown.
Blazer au koti mbili zenye miundo ya kike, blue na black.
Sketi moja inavuka magoti na moja juu ya magoti zenye rangi nyeusi
Gauti moja mid length nyeusi classy
Gauni ya usiku inayositiri vyema (Events za usiku za kikazi)
Viatu
Viatu vyake huwa basic, na kuna kiatu pair moja kwa ajili ya kila tukio. Kiatu kimoja katika capsule kinaweza kuvaliwa katika tukio jingine kikiwa paired na nguo ya tukio hili. Viatu hivi vinakuwa na rangi zinazoendana na rangi nyingine nyingi kama rangi nyeusi, nyeupe, nude. Kwa dada anayefanya kazi katika sekta maalumu capsule yake ya viatu inaweza kuwa pair tano za viatu. Stiletto , high heel sandal , sneaker nyeupe, simple za kufunika mguu, na flat sandals. Unahitaji msaada kutengeneza capsule wardrobe follow @elegancebyree.
Accessories
Ili kuboresha muonekano wa mavazi, accessories ni muhimu. Accessories katika capsule wadrobe lazima ziendane na mavazi na pia zile zenye ubora na zinazodumu. Urembo wa mwili kama hereni na saa uwe na rangi moja.Mfano Lisa ana hivi;
Mkoba mweusi size ya kati kwa ajili ya ofisi.
Mkoba mdogo unaoweza kubebwa mkononi au kuning’inizwa.
Purse au crutch kwa ajili ya jioni.
Saa ya gold
Hereni za pini za gold, hereni ndogo za kuning’inia za gold.
Cheni moja nyembamba ya gold
Scarf moja yenye white, gold and black
Hii ni capsule ya Lisa, katika capsule hii anaweza kupata looks nyingi sana kwa kumix na kumatch nguo za chini na nguo za juu mbalimbali pamoja na viatu. Kama ilivyo katika capsule ya Lisa, ni muhimu rangi za nguo kuendana.
Imeandikwa na @elegancebyree
Related posts
6 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Read More on on that Topic: afroswagga.com/mitindo/fahamu-kuhusu-capsule-wardrobe/ […]
… [Trackback]
[…] Read More on that Topic: afroswagga.com/mitindo/fahamu-kuhusu-capsule-wardrobe/ […]
… [Trackback]
[…] Find More to that Topic: afroswagga.com/mitindo/fahamu-kuhusu-capsule-wardrobe/ […]
… [Trackback]
[…] Read More on that Topic: afroswagga.com/mitindo/fahamu-kuhusu-capsule-wardrobe/ […]
… [Trackback]
[…] Read More here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/fahamu-kuhusu-capsule-wardrobe/ […]
… [Trackback]
[…] Information to that Topic: afroswagga.com/mitindo/fahamu-kuhusu-capsule-wardrobe/ […]