SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

FAHAMU KUHUSU MBUNIFU ALIYE MPA RAY C MUONEKANO MPYA
Mitindo

FAHAMU KUHUSU MBUNIFU ALIYE MPA RAY C MUONEKANO MPYA 

 Tume kuwa tukiona picha mitandaoni kuhusu Ray C na muonekano wake mpya, tukaona sio mbaya kama tutamtafuta mtu au mbunifu aliyepo nyuma ya muonekano huu. Anaitwa Irfan Rizwanali  ni Founder & Celebrity Head stylist at Styling Consultancy, Fashion Influencer na stylist
Afroswagga – Mambo Irfan, tumeona picha kutoka kwa mwanadada Ray C ukiwa wewe ndio ume m’style hongera kwa kazi nzuri Ray C amependeza sana. Kama stylist ulipata ugumu gani na urahisi gani kufanya kazi na Rehema?
Irfan Rizwanali -Styling na kumpiga picha Ray C ilikuwa ni furaha kubwa kwangu. Changamoto niliyokutana nayo ilikuwa kuratibu upigaji picha huo. Kila mtu alikuwa busy na ratiba zao na tulikuwa tunataka kupiga picha kabla 2016 kuisha. Ilikuwa ni kazi ngumu kuleta kila mtu pamoja katika siku moja ili kuweza kupiga picha hizo.
Afroswagga –  Tunamjua Ray C ni mzuri katika mitindo Je alivyo kwambia ana taka kufanya na wewe kazi ni sura gani ilikujia ukitegemea Ray C na yeye ni Icon kwenye Fashion?


Irfan RIzwanali -Ray C amekuwa legend katika tasnia ya muziki, na nimekuwa nikipenda kazi zake tangu ninavyoweza kukumbuka. Tulivyopanga kupiga hizi picha, nilitaka kuonesha utu wake na shauku yake, na kumuonesha tofauti yake kwa njia tofauti na vile watu wanavyomtathmini. Timu yangu na mimi tulifanya utafiti kidogo na kukuta kwamba alikuwa ni mfuasi mkubwa wa Bollywood, hivyo tukaja na dhana ya Indo / African Fusion. Yaani kuchanganya Uhindi na Uafrika. Tukamtafutia mavazi mazuri na kumwambia jinsi ya kukaa katika picha ili kuonesha jinsi alivyo Diva.

Afroswagga – Ray C amekaa muda mrefu mno bila kuonekana katika media au kufanya muziki kwa sasa ana taka kurudi Je umejiandaaje kumrudisha ata rudi kama yule kiuno bila mfupa na zile style zake za kitovu nje au tutegemee nini?

Irfan Rizwanali – Tulifanya majadiliano kadhaa na mikakati juu ya kurudi kwake na tupo katika mipango hiyo, ambayo siwezi kuzungumzia kwa sasa, ni kweli anarudi katika tasnia ya muziki baada ya muda mrefu na sisi tupo kuhakikisha kwamba anarudi kwa mlipuko. Nimesikiliza albamu yake mpya na naweza kusema kwa kujiamini kwamba mashabiki hawatokatwa tamaa.

Afroswagga –  Kama stylist tunauanza mwaka 2017 tutegemee nini je atakuwa huyu huyu Ray C au kuna wengi kutoka kwako tuwategemee na lolote la kumalizia kwa ajili ya watakao soma hii interview.

 Irfan Rizwanali – Tuna mipango mingi kwa ajili ya 2017, Si kwa Ray C tu lakini kwa watu wengi wenye majina makubwa na makampuni ambayo majadiliano yameshaanza na tutatangaza rasmi kila kitu kikithibitika. Sisi daima tunajaribu kuleta kitu kipya na dhana mpya kama Stylists, na tunawahakikishia kuwa; kuna mambo mengi mapya yanakuja, mnachohitaji kufanya ni  kusubiri.
 Tunashukuru kwa kuungwa mkono miaka yote ya kazi zetu na tunatarajia kwamba upendo wenu utaendelea mtaendelea kuunga mkono kazi yetu.
we can’t wait kwa kazi mpya za ray C lakini pia we can’t wait to see more of her fashion this year
Styling Credits
Model @rayc1982
Photography @azhphotography
Makeup by @simplygorgeous_tz
Concept and Styling @irfanrizwanali
Designer @bijoux_trendy
Accessories @manyatta_101
Hair@heaventz
Shoes @lavidoz

Related posts

2 Comments

  1. 대구웨딩홀

    … [Trackback]

    […] Info to that Topic: afroswagga.com/mitindo/fahamu-kuhusu-mbunifu-aliye-mpa-ray-c-muonekano-mpya/ […]

  2. ephedrine for sale

    … [Trackback]

    […] Read More Information here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/fahamu-kuhusu-mbunifu-aliye-mpa-ray-c-muonekano-mpya/ […]

Leave a Reply