SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Fahamu Namna Ya Kujua Sizes Za Handbag Za Aina Ya Hermes Birkin
Mitindo

Fahamu Namna Ya Kujua Sizes Za Handbag Za Aina Ya Hermes Birkin 

Kama wewe ni mpenzi au mnunuaji sana wa designers’ handbags bila shaka jina la Hermès Birkin linaweza lisiwe geni kwako. Dizaini hii ya pochi imejizolea umaarufu kutokana na muonekano wake mzuri na pia kumfanya mtu ajihisi wathamani wakati anapokuwa ameubeba. Collection ya handbags za Birkins huja katika saizi tofauti tofauti kwa kutegemea ukubwa wa sentiminta za upana na urefu wake. Hakuna sheria zinazokubana kuchagua size ya handbag hizi, lakini  kufahamu nini kinaweza kuenea katika mkoba wako ni njia pekee itakayo kusaidia kuchagua size ya mkoba utakao kufaa kwa matumizi yako. Ingawa limited editions zimeshawahi kutengenezwa kipindi cha nyuma (mfano micro edition), sio vibaya leo tukazifahamu size kuu 4 za Hermès Birkins na nini kinafaa kubebeka ndani.

1.       Hermès Birkin 25cm (Mini)

Hii ni size ndogo kabisa yenye upana 25cm na urefu 20cm. Kwasababu ya udogo wake haibebi vitu vingi sana ila sanasana inatumika kwa mitoko ya jioni na ile ambayo itakuhitaji kubeba vitu vidogo vya muhimu.

Nini kinafaa kubebeka:  Simu, wallet ndogo, miwani, funguo na kipodozi mfano; lipstick.

2.       Hermès Birkin 30cm (Small-Medium)

Hii ni saizi ndogo ya kati yenye upana 30cm na urefu 22cm. Pamoja na kuwepo toleo  saizi ya kati (medium 35cm); small-medium ndio saizi inayojulikana ingawa huwa ni ngumu kidogo kutofautisha kati ya small-medium (30cm) na medium (35cm).

Nini kinafaa kubebeka: Simu, wallet, miwani, funguo na kibegi cha make up.

3.       Hermès Birkin 35cm (Medium)

Birkin yenye upana wa 35cm na urefu wa 25 inaonekana kuwa chaguo la wengi na kuwa ndio size inayohitajika na watu wengi zaidi. Kama bado ikitokea  ukapata ugumu kuchagua kati ya Birkin 30cm na 35cm, njia rahisi ni  kuamua kwanza vitu gani utabeba. Kama utalazimika kutembea na iPad au laptop ndogo basi utahitaji kubeba Birkin hii ya 35cm.

Nini kinafaa kubebeka: Simu, wallet, miwani, funguo, kibegi cha make up na iPad au laptop ndogo.

4.       Hermès Birkin 40cm (Large)

Birkin 40cm ndio Birkin ya kwanza kabisa kutengenezwa maalum kwa ajili ya Jane Birkin. Ina upana 40cm na urefu 30cm. Wanawake wengi wamekuwa wakiiona kama ni kubwa sana kwa matumizi ya kawaida ya kila siku, ndio sababu hata ikapelekea size za small-medium (30cm) na medium(35cm) kujulikana zaidi kutokana na uhitaji kuwa mkubwa ukilinganisha na Large size. Hata hivyo size hii ni nzuri zaidi kama unahitaji bag ya kusafiria kwa siku chache.

Nini kinafaa kubebeka: Simu, wallet, miwani, funguo, kibegi cha make up, laptop, charger, kitabu na hata chupa ya maji.

Baada ya kufahamu haya machache, usisahau kuweka comment yako hapo chini na kushare na wengine makala hii.

Imeandikwa na @gift_reinhard

Related posts

5 Comments

 1. download instagram video iphone

  … [Trackback]

  […] Read More on on that Topic: afroswagga.com/mitindo/fahamu-namna-ya-kujua-sizes-za-handbag-za-aina-ya-hermes-birkin/ […]

 2. ufa

  … [Trackback]

  […] There you can find 70786 more Info to that Topic: afroswagga.com/mitindo/fahamu-namna-ya-kujua-sizes-za-handbag-za-aina-ya-hermes-birkin/ […]

 3. weed delivery Toronto

  … [Trackback]

  […] Find More to that Topic: afroswagga.com/mitindo/fahamu-namna-ya-kujua-sizes-za-handbag-za-aina-ya-hermes-birkin/ […]

 4. 티비위키

  … [Trackback]

  […] There you can find 69764 more Information to that Topic: afroswagga.com/mitindo/fahamu-namna-ya-kujua-sizes-za-handbag-za-aina-ya-hermes-birkin/ […]

 5. สล็อต ฝากถอน true wallet เว็บตรง 888pg

  … [Trackback]

  […] Read More on on that Topic: afroswagga.com/mitindo/fahamu-namna-ya-kujua-sizes-za-handbag-za-aina-ya-hermes-birkin/ […]

Comments are closed.